LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 25, 2018

ZIARA YA WAZIRI KANGI LUGOLA KATIKA KITUO CHA POLISI MURIET JIJINI ARUSHA

 Waziri   wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Kangi Lugola akiangalia pikipiki zilizotolewa na wadau wa kupinga vita uhalifu  kwa Kituo cha Polisi Muriet, kilichopo Kata ya Muriet. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’anzi.Waziri Lugola yupo jijini Arusha kwa ziara ya kikazi.
 Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,  Mrisho  Gambo (kulia)  na Kamanda  wa  Polisi  Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’anzi (kushoto) kutembelea  Kituo cha Polisi cha Muriet (kinachoonekana pichani) na nyumba za askari polisi zilizopo katika eneo hilo wakati wa ziara yake jijini Arusha. 
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola(wapili kushoto), alipotembelea nyumba za askari polisi zinazoonekana pichani, katika eneo la Kata ya Muriet,jijini Arusha.Kushoto  ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Ramadhani Ng’anzi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na wananchi wa Kata ya Muriet,  baada ya kutembelea Kituo cha Polisi na nyumba za askari polisi zilizopo eneo hilo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages