China na Afrika Kusini Julai 25, 2018 zimezitolea wito nchi wenza zinazounda kundi la BRICS kupambana na kile kilichotajwa na nchi hizo kuwa ni hatua ya kuvilinda na ushindani wa nje viwanda vya ndani vya nchi moja kupitia ushuru wa forodha.
Nchi mbili hizo pia zimetilia mkazo suala la kukuza biashara ya kimataifa ili kukabiliana na vitisho vya ushuru wa forodha kutoka kwa Rais Donald Trump wa Marekani ambavyo vinatishia biashara ya kimataifa.
Vitisho hivyo vya Trump vimezipa msukumo mpya nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini wa kuimarisha ushirikiano wa biashara. Mkutano huo wa Marais wa nchi zinazounda kundi la BRICS umeanza Julai 25, 2018 Jumatano mjini Johannesburg Afrika Kusini.
Zhang Shaogang Mkurugenzi Mkuu katika Wizara ya Bishara ya China ameuambia mkutano wa nchi wanachama wa kundi la BRICS kuwa ni jukumu la nchi hizo kudhihirisha uwajibikaji wao kuelekea mfumo wa biashara jumuishi ili kulinda uwepo wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) na vilevile kuonyesha msimamo wa wazi na thabiti wa nchi wanachama wa BRICS dhidi ya siasa za kujichukulia hatua za upande mmoja.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇