LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 15, 2018

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA (CPC) ATUA NCHINI APOKELEWA NA NDG. BASHIRU ALLY KATIBU MKUU WA CCM

Ndg Song Tao (Kushoto) Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama cha Kikomunisti cha Watu wa China na mwenyeji wake Ndg Bashiru Ally Kakulwa (Kulia) Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi wakikagua Gwaride maalum la vijana wa Chipukizi wa Chama cha Mapinduzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.CCM 
LUMUMBA, DAR ES SALAAM
Komredi Song Tao Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti Cha China (CPC) amewasili nchini Tanzania na kupokelewa na mamia ya wanachama wa CCM wakiongozwa na Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius  Nyerere Jijini Dar es salaam.
Komredi Song Tao amefanya mazungumzo na Viongozi wa Sekretariati ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba, ambapo ameendelea kusisitiza kuwa CPC itaendeleza ushirikiano na urafiki mzuri na CCM uliosisiwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mao Zedong miaka zaidi ya 50 iliyopita.
Naye Ndg. Bashiru ally Katibu Mkuu wa CCM akimkaribisha Ndg. Tao nchini Tanzania amesema, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinathamini sana uhusiano kati ya CCM na CPC na Uhusiano mzuri sana uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya China na kwa niaba ya CCM amemhakikishia Ndg. Song kwamba ushirikiano zaidi katika Nyanja mbalimbali kwa manufaa ya vyama vyetu na wananchi wa mataifa yetu.
Komredi Song Tao yupo nchini kwa ajili ya Mkutano wa Kidunia wa vyama vya siasa  utakaofanyika siku ya tarehe 17 na 18 Julai 2018, pia atashiriki katika uwekaji wa jiwe la msingi wa Chuo cha Uongozi cha Chama Cha Mapinduzi kitakachojulika kwa jina la Chuo cha Uongozi Cha Mwalimu Julius Nyerere.
Aidha, Komredi Song Tao atatembelea Chuo kikuu cha Dar es Salaam na Stesheni ya Tazara.
Imetolewa na,

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI
OFISI NDOGO LUMUMBA

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages