LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 4, 2018

WAZIRI MKUU AONGOZA KUUAGA MWILI WA MBUNGE WA KOROGWE


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini Kitabu cha Maombolezo ya kifo cha Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Hillary Ngonyani na kuwaongoza waombolezaji kuuaga mwili wa mbunge huyo kwenye Viwanja vya Karimjee jijijini Dar es salam, Julai 4, 2018. 

Dar es Salaam
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Korogwe Vijijini, Bw. Stephen Ngonyani maafufu Profesa Maji Marefu.

Bw. Ngonyani ambaye alifariki dunia Julai 2, 2018 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbi ameagwa leo (Jumatano, Julai 4, 2018) katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa pole kwa wanafamilia, wabunge, wananchi wa Korogwe pamoja na Watanzania kwa ujumla. Amewataka waendelee kumuombea marehemu.

“Natoa pole kwa wake wa marehemu, watoto na nawaomba tuendelee kuwa wavumilivu katika kipindi hiki. Tulimpenda sana lakini Mwenyezi Mungu amempenda zaidi,”.Kwa upande wake, Katibu wa Bunge, Bw, Stephen Kagaigai akisoma wasifu wa marehemu amesema Bw. Ngonyani alizaliwa Mei 25, 1956 katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

Bw. Kagaigai amesema marehemu alianza kuugua Juni 17 mwaka huu na Juni 18 alilazwa katika Hopitali ya Mkoa wa Dodoma na Juni 20 alihamishiwa katika Hopitali ya Muhimbili.Shughuli hiyo ilihudhuriwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi. Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally, Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Wabunge na wanafamilia.
Wapambe wa Bunge wakiwa wameubeba mwiili wa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stehen Hillary Ngonyani kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  na waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Hilary Ngonyani kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam. 
Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza na waombolezaji Katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam wakati wa kuuaga mwiili wa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Hillary Ngonyani.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (wa nne kulia) na Spika wa Bunge Job Ndugai wakisikiliza salamu mbalimbali za waombolezaji kabla ya kuuaga mwiili wa mbunge wa Korogwe Vijijini , Stephen Hillary Ngonyani kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Julai 4, 2018. Wengine kutoka kushoto ni Mbunge wa Vunjo, James Mbatia, Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson , Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi, John Kijazi na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Hillary Ngonyani wakati alipowaongoza waombolezaji katika kuaga mwili wa mbunge huyo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wanafamilia wakati alipowaongoza waombolezaji kuuaga mwili wa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Hillary Ngonyani kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Julai 4, 2018. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda (kushoto) wakati alipoongoza waombolezaji kuuaga mwili wa mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Hillary Ngonyani kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dodoma Julai 4, 2018. Wapili kulia ni Spika wa Bunge Job, Ndugai na wapili kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages