LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 4, 2018

WANAJESHI 30 WA SAUDI ARABIA WAMEANGAMIZWA YEMEN MWEZI JUNI ULIOPITA PEKEE

Wanajeshi wasiopungua 30 wa Saudi Arabia wameangamizwa nchini Yemen katika kipindi cha mwezi Juni uliopita.
Taarifa zinaeleza kuwa, mwezi wa Juni uliopita ulikuwa mbaya mno kwa vikozi vamizi vya Saudia huko Yemen kwani vilipata hasara kubwa mno.
Ripoti za kuaminika zinabainisha kwamba, wanajeshi hao vamizi wa Saudia waliuawa katika operesheni mbalimbali za jeshi la Yemen na vikosi vya kujitolea vya wananchi ambavyo vimekuwa vikipambana na wavamizi hao.
Miongoni mwa maeneo ambayo wanajeshi wa Saudia waliuawa ni yale ya mpakani ikiwemo mikoa ya Najran, Jizan na Asir kusini mwa Saudia.
Hivi sasa jeshi la Yemen na vikosi vya kujitolea vya wananchi vimekuwa vikilenga ngombe na vituo vya muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudia ndani na nje ya Yemen.
Mfalme wa Saudia Salman bin Abdul Aziz al-Saud
Baadhi ya ripoti zinaeleza kuwa, vyombo rasmi vya Saudia vimekuwa vikichuja sana habari za wanajeshi wa nchi hiyo wanaouawa katika vita huko nchini Yemen.
Mashambulio na mauaji ya Saudia dhidi ya raia wasio na hatia wa Yemen yanaendelea kushuhudiwa licha ya miito mbalimbali inayotaka kuhitimishwa jinai hizo dhidi ya raia.
Mashambulio ya anga ya usiku na mchana ya Saudi Arabia dhidi ya Yemen yaliyoanza Machi mwaka 2015 hadi sasa yameshaua maelfu kwa maelfu ya raia na kuwafanya wengine zaidi ya milioni tatu wabaki bila ya makazi.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages