Mwanasheria wa CCM, wakili wa kujitegemea Mwesigwa Zaidi (watatu kushoto) akiwa kwenye kikao cha Wazee wa Jumuiya ya Wazazi tawi la CCM King'azi B, Kata ya Kwembe, jijini Dar es Salaam, jana.
DAR ES SALAAM
Mwanasheria wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wakili wa kujitegemea Mwesigwa Zaidi, amewasihi Wazee wasikubali yavunjwe maadili ya CCM yaliyojengwa na Waasisi na kuendelea kusimamiwa na Katiba na Kanuni za Chama.
Mwesigwa amesema hayo jana wakati akizungumza katika kikao cha Wazee wa Jumuiya wa Wazazi kilichofanyika katika Tawi la CCM la King'azi B, Kata ya Kwembe, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, ambako alihudhuria akiwa mgeni mwalikwa.
Mwanasheria huyo wa CCM amewataka Wazee hao wasiwe waoga kukemea vitendo vya rushwa kwa viongozi wa CCM wanaojihusisha na vitendo hivyo kwa kuwa ni hatarishi kwa uhai wa Chama na kuwataka waunge mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli za kupambana na rushwa, ufisadi na ubadhilifu wa mali za Chama na za serikali kwa kuwa mapambano hayo ni kwa faida yao na kwa vizazi vyao.
kwa upande wao Wazee hao walisema wapo pamoja na Rais Magufuli na kamwe hawawezi kusaliti misingi imara ya maadili ya uongozi iliyoasisiwa na waasisi wa TANU na ASP hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume.
Your Ad Spot
Jul 30, 2018
Home
Unlabelled
WAKILI MWESIGWA AWASIHI WAZEE WA CCM KUSIMAMIA MAADILI YA CHAMA
WAKILI MWESIGWA AWASIHI WAZEE WA CCM KUSIMAMIA MAADILI YA CHAMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇