Mke wa Waziri Mkuu Mhe. Mama Mary Majaliwa akimjulia hali mtoto Anastazia Baki (8) aliyefanyiwa upasuaji wakurekebisha mishipa ya moyo ambayo imekaa vibaya katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Chain of Hope la nchini Uingereza. Mhe. Mama Majaliwa pamoja na wake wa viongozi wa kikundi cha Millennium Group walitembelea kambi hiyo Julai 27, 2018 na kuchangia shilingi milioni nne kwa ajili ya gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto wawili.
Mke wa Waziri Mkuu Mhe. Mama Mary Majaliwa akiwakabidhi hundi ya shilingi milioni nne wazazi wa watoto Anjela Francis (4) na Sabina Mnyango (4) fedha ambazo zimetolewa na kikundi cha wake wa viongozi cha New Millenium Group kwaajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto hao ambao wanatibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Mhe. Mama Majaliwa pamoja na wake wa viongozi walipotembelea kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Chain of Hope ya nchini Uingereza.
Wake wa viongozi wa kikundi cha New Millenium Group wakiongozwa na Mke wa Waziri Mkuu Mhe. Mama Mary Majaliwa wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi mara baada ya kumaliza ziara yao ya kutemblelea kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Chain of Hope ya nchini Uingereza.
Baadhi ya wake wa viongozi wa kikundi cha New Millenium Group wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) akiwaeleza kuhusu ugonjwa wa kiharusi walipoembelea kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Chain of Hope ya nchini Uingereza. Wake hao wa viongozi wamechangia shilingi milioni nne kwa ajili ya gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto wawili.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇