Serikali ya Uturuki imeitisha Marekani kwamba, iwapo Rais Donald Trump wa nchi hiyo hatoikabidhi Ankara ndege mpya za F 35, basi itaiburuza Washington katika mahakama za kimataifa.
Hayo yanajiri katika hali ambayo vyombo vya habari nchini Uturuki vimemnukuu Rais Recep Tayyip ErdoÄźan wa nchi hiyo akijibu vitisho vya Rais Donald Trump wa Marekani hapo jana aliyesema kuwa, Uturuki itakumbwa na vikwazo iwapo haitomuachia huru padri wa Kimarakeni anayeendelea kushikiliwa nchini humo. Akijibu vitisho hivyo amesema kuwa, kamwe nchi yake haitalegeza kamba katika msimamo wake.
Serikali ya Uturuki ilimtia mbaroni Andrew Brunson, mwezi Oktoba 2016 kwa tuhuma za kuhusika na ugaidi, kufanya ujasusi na pia kuwa na mahusiano na harakati ya Fethullah GĂĽlen anayeishi nchini Marekani ambaye anatafutwa na Uturuki. Mahusiano ya Ankara na Washington, yaliingia doa kufuatia hatua ya serikali ya Uturuki kununua mfumo wa makombora wa S 400 kutoka Russia, tofauti zao juu ya makundi ya Kikurdi ya nchini Syria na kadhalika hatua ya Marekani kukataa kumkabidhi Fethullah GĂĽlen, mwanaharakati wa Kiislamu anayetajwa na Ankara kwamba alihusika kupanga jaribio la mapinduzi ya kijeshi la tarehe 15 Julai 2016.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇