Muwakilishi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Casmir Ndambalilo akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Halmashuri ya Manispaa ya Songea Bi.Tina Sekambo wakati wa ziara ya ujumbe kutoka chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari (MAELEZO)
TAGCO na Idara ya Habari MAELEZO Chachu Mageuzi Utendaji wa Maafisa Habari
Frank Mvungi- MAELEZO, Ruvuma
Moja ya Hatua zilizochukuliwa na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Seriklini (TAGCO) na Idara ya Habari (MAELEZO) ni kuweka utaratibu wa kufuatilia namna Maafisa Habari na Mawasiliano wanavyotoa taarifa za miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika Mikoa na Halmashuri .
Akizungumzia jinsi Halmashuri ya Manispaa ya Songea inavyoweka mazingira wezeshi kwa Afisa Habari kutekeleza jukumu hilo, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bi. Tina Sekambo amesema kuwa dhamira yao ni kumpatia nyenzo zote muhimu katika kutekeleza majukumu yake ya kutoa taarifa za miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa manufaa ya wananchi na wamekuwa wakifanya hivyo kadiri rasilimali zinavyopatikana.
”Mimi natambua umuhimu wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu miradi ya maendeleo na katika hili Halmashuri yetu imeweka mkazo katika kumpatia vitendea kazi Afisa Habari wetu ili atekeleze jukumu la kutoa taarifa kwa wananchi" Alisisitiza Bi. Sekambo
Akifafanua amesema kuwa Halmashuri hiyo itaendelea kuwekeza katika kuimarisha mfumo wa mawsiliano kati ya Serikali na wananchi kwa kutambua numuhimu wa suala hilo wamekuwa wakimshirikisha Afisa Habari katika kila jambo ili kumjengea uwezo katika kutoa taarifa kwa wananchi hasa za miradi ya maendeleo.
Naye Kiongozi wa ujumbe huo Bi Gaudensia Simwanza alisisitiza kuwa kuna umuhimu wa kuwaruhusu maafisa hao kushiriki katika mafunzo mbalimbali na kikao kazi ili kuwaongezea ujuzi katika kuisemea Serikali.
Ziara ya ujumbe huo imefanyika katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ikilenga kuhamasisha maafisa Habari kuongeza kasi katika kuisemea Serikali hasa kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli ikiwa inasisitiza utoaji wa huduma bora kwa wananchi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wakati na ikilenga kunufaisha wananchi wanyonge.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇