LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 16, 2018

RIPOTI YA UN: MAELFU YA WATU WAMEKUWA WAKIMBIZI AL HUDAYDAH, YEMEN

Ripoti mpya iliyotolewa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu nchini Yemen imeeleza kuwa karibu familia elfu 35 katika mkoa wa al Hudaydah wamekuwa wakimbizi na ni karibu watu elfu 20 miongoni mwao pekee ndio waliopokea misaada ya kibinadamu. 
Ripoti hiyo imetolewa na ofisi hiyo ya Umjoja wa Mataifa kwa kushirikiana na kundi la wanaharakati wa masuala ya kibinadamu baada ya kushuhudia hali mbaya ya raia huko Yemen kuanzia tarehe 4 hadi 13 mwezi huu wa Julai. Ripoti hiyo aidha imeashiria mashambulizi ya makombora na ya anga yanayoendelea kufanywa na Saudi Arabia katika maeneo mawili ya raia huko al Tuhaita na Zubaid katika mkoa wa al Hudaydah.
Saudi Arabia inaendelea kushambulia makazi ya raia Yemen
Wakati huo huo imebainika kuwa shughuli za bandari mbili za al Hudaydah na al Salif zinaendelea ingawa njia za kuelekea kwenye bandari na uwanja wa ndege wa mji huo zingali zimefungwa.  
Saudi Arabia ikiungwa mkono na Marekani, Imarati na nchi kadhaa waitifaki wake, Machi 26 mwaka 2015 ilianzisha uvamizi wa kijeshi huko Yemen na kuizingira nchi hiyo baharini, nchi kavu na majini. 

3 comments:

  1. This post is great! I linked your website on my Twitter.
    Hope that my friends will love your writing too.
    Good luck for the future.

    ReplyDelete
  2. Brilliant post. I linked your website on my Twitter. Hope my followers will consider it interesting
    also. Good luck.

    ReplyDelete
  3. Good post. I shared your website on my Tumblr. Hopefully my followers would consider it helpful
    also. Have a nice day. Cheers.

    ReplyDelete

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages