LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 16, 2018

ERITREA YAFUNGUA TENA UBALOZI WAKE NCHINI ETHIOPIA



Eritrea imefungua tena ubalozi wake nchini Ethiopia baada ya nchi hizo mbili jirani kumaliza uhasama wa miongoni miwili kuhusu mpaka.
Ubalozi wa Eritrea umeanza shughuli zake upya leo katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa katika sherehe iliyohudhuriwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed na Rais wa Eritrea Isaias Afwerki.
Viongozi hao wawili walipandisha kwa pamoja bendera ya Eritrea ndani ya jengo la ubalozi huo huku wakisisitiza tena azma yao ya kuimarisha amani baina ya mataifa yao.
Kiongozi wa Eritrea aliwasilia Addis Ababa Jumamosi iliyopita kwa safari ya siku tatu na amerejea nyumbani leo baada ya sherehe hiyo.
Isaias Afwerki ameitembelea Ethiopia siku chache tu baada ya Abiy Ahmed kutembelea mji mkuu wa Eritrea, Asmara ambapo wawili hao waliafiki kuanzusha tena uhusiano wa kidiplomasia.


Eritrea ilijitenga na Ethiopia mwaka 1993  na kukata uhusiano wa pande mbili na hivyo kupelekea Ethiopia ikose njia ya bahari. Mwaka 1998 kuliibuka vita vikali na mzozo wa mpakani baina ya nchi hizo ambao ulipelekea watu zaidi ya 80,000 kupoteza maisha na malaki kuachwa bila makazi.
Mwaka 2000 Umoja wa Mataifa ulizipatanisha pande mbili hizo na kusema eneo la mpakani lililokuwa likizozaniwa ni milki ya Eritrea lakini mapatano hayo ya amani hayakutekelezwa baada ya Ethiopia kuyapinga. Hatimaye mwezi uliopita wa Juni Waziri Mkuu wa Ethiopia aliwashangaza wengi alipokubali mapatano hayo ya amani na hivyo kuhitimisha uhasama baina ya pande mbili hizo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages