LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 22, 2018

RAIS ROUHANI: TRUMP USICHEZE NA MKIA WA SIMBA, JIBU LA IRAN LITAKUWA KALI

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, sambamba na kubainisha kwamba, Iran sio nchi ya uchokozi na inafuatilia udiplomasia, amesisitiza kwamba, nchi hii haina ugomvi na yeyote, lakini maadui wanatakiwa kufahamu kwamba kufanya vita na Iran ni kuingia katika vita kubwa na kufanya amani na Iran ni kufanya amani kubwa.
Rais Rouhani ameyasema hayo leo katika kongamano la wawakilishi wa Iran nje ya nchi ambapo akiihutubu Marekani na kujibu madai yaliyotolewa na viongozi wa Washington kwamba Iran haitouza mafuta nje ya nchi amesema, rais wa Marekani anatakiwa kufahamu kwamba, dhamana ya amani imekuwepo katika eneo kwa kipindi chote cha historia, hivyo Trump hatakiwi kucheza na mkia wa simba, kwa sababu jibu la Iran litakuwa la kukatisha tamaa. Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria siasa za ubaguzi zinazotekelezwa na ikulu ya Marekani (White House) na kusema, hii leo uongozi wa Marekani na kwa njia ya wazi kabisa unafumbia macho heshima na izza ya Waislamu ambapo umetangaza vita dhidi ya Waislamu bilioni moja na milioni 500 duniani kwa kuchezea heshima ya Quds Tukufu iliyoko katika mioyo ya Waislamu kwa lengo tu la kuuridhisha utawala mmoja ghasibu.
Rais Donald Trump wa Marekani
Akibainisha kwamba utawala wa Kizayuni umejengeka juu ya msingi wa uvamizi, ukaliaji mabavu, hiana, kuwafanya watu kuwa wakimbizi, kuua watoto, wanawake na wazee, amesema kuwa, haijawahi kutokea Wazayuni na serikali ya Marekani kukiri wazi kwamba hawatambui serikali yenye jina la Palestina au kwamba Quds Tukufu haihusiani na Waislamu. Kadhalika Rais Hassan Rouhani amesema kuwa, Iran daima imekuwa ikisisitizia katika mazungumzo na nchi za Kiarabu na majirani wa Palestina, kwamba utawala wa Kizayuni sio utawala wa kutumia dalili wala mazungumzo ya mantiki. Ameongeza kwamba, kufanyika makongamano hakuwezi kurejesha ardhi za Palestina zilizoporwa na utawala huo wala kuwarejesha makwao wakimbizi wa Kipalestina, na hii leo wote wanakubaliana na suala hilo. Pia amezungumzia kufeli mtawalia njama za Marekani dhidi ya Iran katika miaka 40 iliyopita na kusema kuwa, ushawishi wa Iran katika eneo la Mashariki ya Kati na dunia haufungamani na miaka hii pekee, bali hii leo msingi wa stratijia ya Iran unaanzia mashariki hadi bara Hindi, kutoka magharibi hadi Bahari ya Mediterranean, kusini hadi Bahari ya Hindi na Bahari Nyekundu na kaskazini mwa Asia, Asia ya Kati na Caucasus.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages