LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 23, 2018

PAPA AITAKA JAMII YA KIMATAIFA KUKOMESHA MAAFA YA WAHAJIRI

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani ameitolea wito jamii ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti za kuzuia kukaririwa maafa ya wahajiri katika maji ya bahari ya Mediterania.
Papa Francis amezitaka taasisi za kimataifa zijiandae kikamilifu  kuchukua hatua za lazima ilikuzuia kukaririwa maafa ya aina hiyo kwa kuheshimu haki na heshima ya kila mtu. Kiongozi wa Kanisa Katoliki ameeleza mshikamano wake na wahajiri ambao wamepoteza maisha katika bahari ya Mediterania wakiwa njiani kuelekea Ulaya. 
Amesema kuwa katika wiki za karibuni kulitangazwa habari za kusikitisha kuhusu kuzama boti zilizokuwa zimebeba wahajiri katika bahari ya Mediterania na kuongoza kuwa anatoa mkono wa pole kwa raia hao na familia zao kufuatia tukio hilo.
Wahajiri wakijaribu kunusuru maisha yao baada ya boti yao kuzama  katika maji ya Mediterania 
Hii ni katika hali ambayo Matteo Salvini Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia hivi karibuni alijibu msimamo wa kanisa Katoliki kuhusu ulazima wa kuwapokea wahajiri na kuepukana na mienendo isiyofaa dhidi yao akieleza kuwa: Watafanya jitihada za kunusuru maisha ya raia hao lakini akaongeza kuwa sambamba na hilo wanajaribu pia kupunguza safari zenye hatari kubwa na zenye kusababisha vifo katika maji ya bahari ya Mediterania.  

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages