LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 26, 2018

NDOTO YA POMPEO KUHUSU KUSALIMU AMRI IRAN NCHIN AMBAYO KATU HAIFUATI MATAKWA YA MAREKANI

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kwa mara nyingine ameonyesha wazi mwelekeo ulio dhidi ya Iran wa nchi yake na kudai kuwa: "Mashinikizo ya Marekani yamebadilisha mwenendo na sera za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika eneo la Mashariki ya Kati."
Mike Pompeo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani siku ya Jumatano katika kikao cha Kamati ya Sera za Kigeni ya Bunge la Senate alifafanua sera za Marekani kuhusu Iran na kudai kuwa: "Iran ya sasa si sawa na ya miezi mitano iliyopita na hili linatokana na mashinikizo ya kifedha pamoja na Marekani kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA." Waziri huyo wa mambo ya nje wa utawala wa Trump ameendelea kudai kuwa:"Marekani inapinga Iran kuwa na uwezo wa kurutubisha madini ya urani."
Aidha Jumapili wiki hii, Pompeo akizungumza katika mjumuiko wa kijikundi cha wapinzani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika jimbo la California kwa mara nyingine alibainisha mitazamo yake dhidi ya Iran na kusema, Iran ni inchi inayopinga kikamilifu kambi ya Maghairibi . Aliongeza kuwa Ikulu ya White House, kwa ushirikiano na nchi nyingine na pia kupitia mashinikizo na sera maalumu, inalenga kuhakikisha kuwa uuzaji mafuta ya petroli ya Iran katika soko la kimataifa unafika sufuri.
Utawala wa Trump na maafisa wake wa ngazi za juu wenye misimamo mikali na ya kufurutu ada dhidi ya Iran, wanatumia mbinu mbalimbali ili kuishinikiza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika pande zote na kulazimisha Iran iketi katika meza ya mazungumzo kwa masharti yao.
Suala linalofuatiliwa na utawala wa Trump ni kuhakikisha kuwa Iran inakuwa tegemezi kwa Marekani na pia Marekani inapata ushawishi ndani ya Iran na kuipokonya Tehran vyanzo vya nguvu na uwezo wake. Kimsingi utawala wa Trump unafuatilia lengo kuu la kuuangusha mfumo na utawala wa Kiislamu nchini Iran.
Kujiondoa Marekani katika mapatano ya nyuklia ya Iran, JCPOA, kuzidisha mashinikizo ya kiuchumi na kisiasa na kushadidisha vita vya kisaikolojia ni mambo yanayofanywa ili, kwa dhana potofu ya wakuu wa White House, kuilazimisha Iran kufanya mazungumzo na Marekani.
Bahram Qassemi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran
Uzoefu wa miaka 40 tokea baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu umewaonyesha wengi, hasa wakuu wa Marekani kuwa Iran haiwezi kusalimu amri mbele ya mashinikizo. Iran, kwa vyovyote vile haitakubali kupoteza uhuru na kujitegemea kwake kisiasa, kiuchumi, kijeshi na kiutamaduni.
Hii leo utawala wa Trump pia hautafanikiwa katika mbinu yake ya kutumia vitisho na mashinikizo ili kuilazimisha Iran ifanye mazungumzo.
Ni kwa msingi huu ni ndio maana Bahram Qassemi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran akijibu matamshi ya hivi karibuni ya maafisa mbalimbali wa Marekani ambayo yameandamana na vitisho na kutaka mazungumzo na Iran akasema: "Marekani inapaswa kuelewa kwamba zama za siasa za kibabe, ujuba na kuyapima mambo yote kwa mtazamo wa aina moja zimepita na kuyoyoma. Iran haiamini maneno na mienendo ya Marekani." Aidha amewaambia maafisa wa nchi hiyo wasahau kabisa kufanya mazungumzo na Iran kwa mienendo wa kijuba na chini ya vitisho na wala wasikariri tajiriba iliyofeli na kushindwa. 
Pengine lugha hiyo ya vitisho na wakati huo huo kutaka kufanya mazungumzo na Iran imeweza kutumiwa kwa mafanikio na Marekani katika kuamiliana na baadhi ya nchi, lakini kile wanachopaswa kuelewa wakuu wa Washington ni kuwa, Iran ni nchi yenye ustaarabu wa maelfu ya miaka na ina misingi imara ya nguvu na uwezo na hivyo haiwezi kuwa mateka wa nadharia ya mashinikizo ya Marekani. 
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo hii, kwa baraka za mshikamano na umoja wa kitaifa, imeweza kupata nguvu na uwezo mkubwa katika nyuga mbalimbali. Iran ina uwezo mkubwa wa kijeshi na kujihami, na nafasi muhimu ya kistratijia na imekuwa na nafasi athirifu katika matukio ya eneo la Mashariki ya Kati. Iran haitegemei madola makubwa ya kibeberu duniani katika uwezo na nguvu zake kieneo. Hii leo zama za ubabe, ubeberu na sera za kambi moja zimefika ukingoni na katika hali kama hii, serikali zinazojitegemea haziwezi kuwa mateka wa madola ya kibeberu.
Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ)
Leo Iran inaendelea kupata ushindi dhidi ya Marekani katika uga wa kisiasa na kisheria duniani. Ni katika fremu hii ndio maana Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu, (ICJ) ikatoa jibu chanya kuhusu mashtaka yaliyowasilishwa na Iran dhidi ya Marekani. Rais Hassan Rouhani wa Iran katika kikao cha Baraza la Mawaziri Siku ya Jumatano ameashiria mashtaka yaliyowasilishwa na Iran katika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) kuhusu hatua zilizochukuliwa na Marekani dhidi ya Iran na kueleza kuwa, akthari ya nchi duniani zimelaani na kuzitaja hatua hizo za Marekani kuwa si sahihi au kwa uchache zimeeleza kusikitishwa na hatua hizo.  Alisema Marekani inapasa kuwa na tahadhari mkabala na vitendo na mipango inayotekeleza kufuatia onyo lililotolewa na mahakama hiyo dhidi yake. Rais Rouhani aidha amesema hatua ya ICJ inaonyesha kufanikiwa msimamo wa Iran wa kusimama kidte na kuongeza kuwa  Iran itasimama kidete dhidi ya njama za maadui katika sekta zote.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages