Thursday, July 19, 2018

NDEGE ZISIZO NA RUBANI ZA YEMEN ZASHAMBULIA SHIRIKA LA MAFUTA LA SAUDIA, MJINI RIYADH

Msemaji wa Jeshi la Yemen amesema baada ya ndege zisizo na rubani za nchi hiyo kushambulia kwa makombora Shirika la Mafuta la Saudi Arabia (ARAMCO) kwamba, operesheni ya jeshi la Yemen kwa kutumia ndege hizo zisizo na rubani, zimeleta mabadiliko makubwa katika vita dhidi ya maadui.
Sharaf Luqman amefafanua kuwa, mafanikio ya hujuma za makombora za Wayemen katika kulilenga Shirika la Mafuta la Saudia (ARAMCO) yanahesabiwa kuwa ni mwanzo wa uwezo katika hatua mpya ya mapambano dhidi ya maadui. Msemaji wa Jeshi la Yemen amebainisha kwamba, katika mustakbali wa karibu, kutashuhudiwa operesheni zaidi za kushtukiza za ndege zisizo na rubani pamoja na makombora ya jeshi na harakati ya wananchi ya Answarullah dhidi maadui. Wakati huo huo Abdullah Hassan al-Jafri, Msemaji wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Yemen ameiambia kanali ya televisheni ya al-Mayadin ya nchini Lebanon akisema kuwa, katika operesheni za ndege zisizo na rubani zilizofanyika jana usiku, Shirika la Mafuta la Saudia lilishambuliwa kwa makombora na ndege hizo na kuteketea kwa moto.

Ndege isiyo na rubani ya Yemen

Kikosi cha ndege zisizo na rubani cha jeshi la Yemen pamoja na harakati ya Answarullah kilishambulia kwa kombora aina ya Swamaad-2 lililobebwa na ndege isiyo na rubani, kiwanda cha kusafishia mafuta cha Shirika la Mafuta la Saudia ARAMCO) katika mji mkuu wa nchi hiyo Riyadh. Hii ni mara ya kwanza kwa jeshi la Yemen kutumia ndege zisizo na rubani kushambulia kwa kombora la masafa marefu la Swamaad-2 ardhi ya Saudia. Shirika la Kitaifa la Mafuta la Saudi Arabia limekiri kutokea moto mkali katika eneo lililolengwa. Mashambulizi ya makombora ya Wayemen dhidi ya maeneo muhimu ndani ya Saudia, yanaonyesha kuongezeka uwezo zaidi wa jeshi la Yemen na harakati ya Answarullah, suala lililowafanya viongozi wa muungano vamizi wa Saudia kuchanganyikiwa na kuelekezeana tuhuma.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Mdau, andikamaoni yako hapa yasaidie kujua wewe unafikiri nini kuhusu posti hii. Tafdhali, Maoni yako yasiwe ya uchochezi wa aina yoyote.. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

CCM Blog. Powered by Blogger.