LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 25, 2018

MAKAMU WA RAIS AZINDUA SHAMBA LA MITI HIFADHI YA MISITU IYONDO-MSIMWA HUKO ILEJE

 Kikundi cha Ngoma cha Sange kikitumbuiza ngoma ya Ling'oma wakati wa kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye kijiji cha Sange wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Songwe.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya shamba la Misitu kutoka kwa Mkurugenzi wa Mipango-Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Bw. Mohamed Kilongo kwenye uzinduzi wa shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe.

NA OMR, ILEJE
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  amezindua shamba la miti katika hifadhi ya Misitu Iyondo Mswima lililopo Katengele wilayani Ileje mkoani Songwe ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Songwe.
Shamba hilo lililo chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ni moja kati ya mashamba mapya yakiwemo Biharamulo (Chato Geita), Buhigwe (Kigoma) na Mpepo (Mbinga, Ruvuma).
Akisoma taarifa ya Shamba hilo kwa Makamu wa Rais, Mkurugenzi wa Mipango –Wakala wa Misitu Tanzania Bw. Mohamed Kilongo amesema kuwa mpaka shamba la miti la Iyondo Mswima limeweza kutoa ajira kwa wananchi 400 katika msimu wa kupanda miti, pia shamba limetoa ajira zingine 200 wakati huu wa maandalizi ya bustani ya miti, hekta 201 zimepandwa miti kama sehemu ya upanuzi wa mashamba ya miti ya Serikali ambapo bustani yenye jumla ya miche 430,000 kwa ajili ya upandaji miti wa mwaka 2018/2019.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Katengele ambapo shamba la misitu la Serikali Iyondo Mswima limezinduliwa, Makamu wa Rais amewataka wananchi hao kutunza na kuyalinda mazingira kwa kupanda miti kwa wingi ambapo kila mwaka wananchi watapewa miche 50,000 na Wakala wa Huduma za Misitu wa Serikali.
Makamu wa Rais pia alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Sange ambapo aliwaambia wananchi wa kijiji hicho kuwa Mungu amewapa rasilimali nzuri sana hivyo hawana budi kuyatunza.
Makamu wa Rais amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ileje kuhakikisha Maafisa Ugani wanashuka kwa wananchi na kutoa ushauri namna ya kufanya shughuli za kilimo vizuri.
Makamu wa Rais amesema Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 1.5 katika bajeti mwaka huu iliyopita kwa ajili ya kujenga hospitali ya wilaya ya Ileje.
Makamu wa Rais amesema mkoa wa Songwe utapata watumishi 270 katika Sekta ya Afya, na kwenye sekta ya elimu, walimu wengi wameajiriwa mwaka huu ambapo Songwe nayo itapata walimu wapya.
Makamu wa Rais ameandika historia kwa kuwa kiongozi wa ngazi za juu kufika katika vijiji vya Katengele na Sange.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa kijiji cha Katengele mara baada ya kuzindua shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya shamba la Misitu kutoka kwa Mkurugenzi wa Mipango-Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Bw. Mohamed Kilongo kwenye uzinduzi wa shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa kijiji cha Katengele mara baada ya kuzindua shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe.
 Makamu wa Rais akikata utepe kama ishara ya kuzindua shamba la miti katika hifadhi ya Misitu Iyondo Mswima lililopo Katengele wilayani Ileje mkoani Songwe


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbuge wa Jimbo la Ileje Mhe. Janeth Mbene mara baada ya kuwasili kwenye uzinduzi wa shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia  wakazi wa kijiji cha Sange wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe.(PICHA NA OMR)

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages