LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 2, 2018

JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI - WATANZANIA WENYE CHIMBUKO (ROOTS) LA MUSOMA VIJIJINI WAAMUA KUSHIRIKIANA NA NDUGU ZAO WA VIJIJINI KUTOKOMEZA UMASKINI WAO

Leo, Jumatano, 2.5.2018, Wafanyabiashara, Wafanyakazi, Wasomi na Wataalamu waliozaliwa au wazazi waliozaliwa Kijiji cha Mkirira, Kata ya Nyegina, Jimbo la Musoma Vijijini wameshirikiana na Mbunge wa Jimbo (Prof Sospeter Muhongo), Diwani wa Kata (Mhe Majira) na Wanakijiji wa Kijiji cha Mkirira kuchanga jumla ya Tshs 1.6 Milioni na Mifuko ya Saruji 238 kwa ajili ya UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA MKIRIRA. Michango inaendelea.

Lengo ni kukamilisha Jengo  hilo kabla ya Desemba 2018.
Jimbo limebuni mbinu mpya za kushirikiana na Serikali kuleta maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii kwa kasi. Miradi ya Elimu, Afya na Kilimo Jimboni inashirikisha MICHANGO na NGUVU za WANANCHI walioko ndani na nje ya Jimbo.

Ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya Elimu na Afya vimewekewa uzito mkubwa sana. Upanuzi wa wigo wa mazao ya chakula na biashara unafanyika kwa kuhamasisha KILIMO cha kisasa. UVUVI na UFUGAJI wa kisasa vinapigiwa kampeni kubwa Jimboni.

Wapenda maendeleo ya ndugu na jamaa zao wanaoishi vijijini wameamua kuanzisha UMOJA miongoni mwao ili kuchangia MAENDELEO kwa VITENDO vijijini walikozaliwa au wazazi wao walikozaliwa - wameamua kuwa WADAU wa MAENDELEO ngazi ya kijiji. TUNAWASHUKURU.
Zifuatazo ni picha zaidi za kikao cha Mbunge wa Jimbo, Diwani na Wanakijiji walioshiriki kuchangia vifaa vya ujenzi

Ofisi ya Mbunge
www.musomavijijini.or.tz

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages