Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu Yussuf Makamba akimnadi Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Kinondoni Said Mtulia, katika mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo katika Viwanja vya Biafra Jijini Dar es Salaam.
"Wewe Kijana unatosha" akasema Makamba
Mbunge wa Mtela Livingistone Lusinde na Mbunge mwenzake wakituza Mzee Makamba baada ya kunogewa na hotuba yake wakati akimnadi Mtulia
Mzee Makamba akiwa ameileta jukwaani familia ya Mtulia, mke na watoto
Mke wa Mtulia akimuombea kura mumewe jukwaaniMwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akimpongeza Msanii Kalapina alipopita mbele yake wakati akienda kukabidhi kadi yake ya chama cha ACT-Maendeleo na kutangaza kujiunga CCM wakati wa mkutano huo
Msanii Kalapina akikabidhi kadi yake ya ACT-Wazalendo kwa Katibu Mkuu wa CCM mstaafu Yussuf Makamba wakati wa mkuatno huo
Mzee Makamba akioyesha kadi hiyo baada ya kukabidhiwa na Msanii Kalapina
Masanii Kalapina akitangaza rasmi kuhamia CCM baada ya kukabidhi kadi yake ya ACT- Wazalendo wakati wa mkutano huo
Naibu Spka wa Bunge Akson Tulia (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Slyvia Kate Kamba na Mwenyekiti wa UWT Tanzania Gaudencia Kabaka (kulia) wakati wa mkutano huo
Baadhi ya viongozi waliokuwa Jukwaa Kuu
Mwenyekiti wa Chipukizi wa CCM Taifa Nimka Lameck (kushoto), akiwa na Mbunge Mchungaji Getrude Rwakatale wakati wa mkutano huo. Kulia ni david kafulia ambaye amejiunga na CCM hivi karibuni
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa akifurahia jambo wakati akiwa kwenye mkutano huo
Baadhi ya wabunge wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo
Baadhi ya wasanii wakiwa kwenye gari la TOT wakati wa mkutano huo
Makanda wa CCM wakiwa kwenye gari la TOT wakati wa mkutano huo
Mgombea Ubunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CCM said Mtulia akijadili jambo na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni wakati wa mkutano huo. Kushoto ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Mndolwa
Mwenyekiti wa zamani wa UVCCM mbaye sasa ni Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Mhandisi Hamadi Masauni na Mwenyekiti wa Chipukizi wa CCM Taifa, Nimka Lameck wakifuatilia hali ya mambo katika mkutano huo
Mwenyekiti wa zamani wa UVCCM mbaye sasa ni Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Mhandisi Hamadi Masauni akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Chipukizi wa CCM Taifa, Nimka Lameck wakatika mkutano huo
Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali (wapili kulia) akifurahia jambo wakati wa mkutano huo
Katibu Mkuu wa UWT Taifa Amina Makilagi (wapili kulia) ni miongoni mwa viongozi wa CCM waliohudhuria mkutano huo
Baadhi ya makada wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo
Jokate Mwengelo kutoka Makao Makuu ya UVCCM akisalimia na kijana mwenzake wa UVCCM walipokutana kwenye mkutano huo
Makada wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo
Mbunge wa Mtela na Mjumbe wa NEC kupitia Wagunge akimuombea kura Mtulia wakati wa mkutano huo
Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM said Mtulia akiomba kura kwa wananchi wakati wa mkutano huo
Wananchi na mashabiki wa CCM wakimshangilia Mtulia alipokuwa akiomba kura wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo katika Viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇