Na Mwandishi Maalum
TUME yaTaifa ya Uchaguzi (NEC)
imetoa orodha ya wanachama 15
wa vyama vya siasa walioteuliwa kugombea ubunge katika majimbo ya Singida Kaskazini na Longido.
Tume pia
imetoa orodha ya majina ya wanachama wengine 15
wa vyama mbalimbali ambao wamejitokeza kugombea udiwani katika uchaguzi mdogo unaofanyika kwenye
kata sita.
Walioteuliwa kugombea ubunge katika jimbo la
Longido ni Kisiongo Mayasek Olokuya (CUF), Francis Ringo (CCK), Dk Steven KIruswa
(CCM), Mgina Mustafa (AFP), Godwin Sarakikya (ADA TADEA), FeruziyFuruziyson
(NRA), Ngilisho Paul (Demokrasia Makini), Simon Bayo (SAU) na Robert Lukumy
(TLP).
Waliojitokeza kugombea ubunge katika jimbo la
Singida Kaskazini ni Omari Sombi (AFP), DalphinaMlelwa (CUF), Monko Joseph (CCM),
David Djumbe (Chadema), Aloyce Nduguta (ADA TADEA) na Mchungaji Yohana Labisu
(CCK)
Katika uteuzi huo pia
kuna walioteuliwa kugombea udiwani katika kata
ya Kimandolu ambako kuna wanachama wa vyama vitano vya Gaudence Lyimo (CCM), Rashid
Nyawaya (CUF), Hamis Mgoya ( NRA), RAmadhani Mcharo (Demokrasia Makini),
na Shafii Kiktunda (SAU).
Katika kata ya Kihesa Halmashauri ya Iringa
Mjini ameteuliwa Sawani Juli (CCM), Kata ya Keza wilayani Ngara walioteuliwa ni
Eradius Bitemele (NCCR Mageuzi), Bakundukize Gwaibondo (CCM), Philipo Bazubwenge
(CUF). Kata yaKuruiwilayaniKisarawewagombeaniKunikuniSalumu (CCM)
naKikumbiMwalimu (CUF),
Kata
ya Bukumbi wilaya ya Uyui wagombea ni Kasoga Sizya (CCM), Edward Msigalawa (CUF) wakati
kata ya Kwagunda wilaya ya Korogwe walioteuliwa ni Said Shenkawa (CCM) na Yusuf
Senkawawa CUF.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇