LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 31, 2017

RUGIMBANA AAHIDI KUENDELEA KUMUUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI

Furaha John, Dodoma
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jodarn Rugimbana ameahidi kuwa raia mwaminifu na mtiifu kwa Rais Dk. John Magufuli wakati wote ili kuhakikisha malengo yote yaliyopangwa na serikali yanatimia.

Rugimbana ameyasema hayo leo mjini Dodoma wakati akikabidhi ofisa na kwa mkuu wa mkoa mpya wa mkoa wa Dodoma Dk. Binilithi Mahenge.

Kuhusu mabadiliko hayo Rugimbana amesema, amesema Rais aamefanya vema, na kwataka wafanyakazi kumpa ushirikiano wa kila aina mkuu huyo mpa wa mkoa ili aweze kutekeleza vema kazi zake.

Ameeleza kuwa, anakwenda uraiani lakini jukumu lake kubwa sasa itakuwa ni kulipa fadhila kwa Magufuli kwa kumchagua kuwa miongoni mwa wasaidizi wake wa kwanza katika serikali yake aliyoiunda mwaka 2015.

Pia aliwapongeza na kuwasifu wakuu wa wilaya zote Saba za Dodoma kuwa ni timu nzuri na wachapakazi wa kutumainiwa.

Kuhusu, mchakato wa serikali kuhamia Dodoma chini ya usimamizi wa Ofisi ya Waziri mkuu, Rugimbana alisema, unakwenda vizuri, mambo yote yako sawa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali.

Rugimbana, ameishukuru timu yote ya mkoa pamoja na waandishi wa habari kwa ushirikiano mkubwa uliowezesha kazi yake kuwa rahisi katika kipindi chote cha uongozi wake.

Kwa Mkoa wa Dodoma, Dk. Mahenge amesema, atamuenzi Rugimbana kwa kusimamia na kuyafuatilia mambo yote yaliyofanywa kwa kuwa no ni maelekezo ya timu aliyokuwa akifanya kazi nayo.

Pia ameahidi kuhakikisha anasimamia vyema utekelezaji wa Ilani ya CCM, katika kuhakikisha kero za wananchi zinatatuliwa kwa wakati.

Dk. Mahenge, ameomba ushirikiano wa hali na mali kutoka kwa watumishi wa Dodoma, ili wote kwa pamoja waweze kufanikisha kuiletea Dodoma maendelea kwani bila ushirikiano kamwe hakutakuwa na miujiza.

Makabidhiano hayo yamefanyika kufuatia mabadiliko ya viongozi wakiwemo wakuu wa mikoa yaliyofanywa wiki iliyopita  na Rais, Dk. John Magufuli ambapo Rugimbana ni miongoni mwa wakuu wa mkoa walioachwa katika uteuzi huo.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages