Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo, leo amezindua kwa kishindo kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Mbweni, Wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, akifuatana na viongozi mbalimbali wa Chama akiwemo Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe. Pichani, Mpogolo akimnadi mgombea wa Udiwani katika Kata hiyo kwa tiketi ya CCM, Hashim Mbonde katika mkutano uliofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi ya afisa Mtendaji Kata ya Mbweni. Kumradhi, Kutokana na muda hatukuweza kuweka maelezo kwenye picha zote, tafadhali pitia moja baada ya nyingine utapata taswira nzima ya shughuli hiyo nzito. Picha zote na Bashir Nkoromo |
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇