Katibu
wa Hakmashauri kuu Idara ya Itikadi na Uenezi Humphrey Pole Pole
akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM Wilaya ya Kilombero katika mkutano wa ndani uliofanyika Julai 28, 2017, katika Kata ya Kidatu akiwa katika ziara ya Kichama mkoani Morogoro.
KIDATU, MOROGORO
Wajumbe
wa kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya kidatu
wamejiuzulu nafasi zao za uongozi kwa pamoja na kuomba radhi wanachama
kwa makosa ya kushindwa kutoa uongozi madhubuti.
Akiwa
katika ziara ya kichama mkoa wa Morogoro Wilaya ya Kilombero kata ya
Kidatu, leo tarehe 28 Julai 2017, Katibu wa Halmashauri kuu Itikadi na
Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu H.H. Polepole alifanya kikao
cha ndani, alipata fursa ya kuzungumza, kusikiliza na kutatua
changamoto mbalimbali za wanachama.
Katika
kikao hicho kilichohusisha Wanachama, Viongozi wa Mashina, Halmashauri
kuu za Matawi na Kamati ya siasa ya kata ya Kidatu, Ndugu Polepole
aliambatana na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiwemo Katibu
wa Chama Cha Mapinduz(CCM) Mkoa wa Morogoro, Katibu wa Chama wilaya,
Mkuu wa mkoa wa morogoro na mkuu wa wilaya ya kilombero.
Wakati
wa kikao hicho kilichoongozwa na Ndugu Polepole baada ya malalamiko na
shutuma nyingi kutoka kwa wanachama dhidi ya viongozi wa CCM kata ya
kidatu ikiwemo kushindwa kusimamia uchaguzi wa matawi, kushindwa
kusimamia rasilimali za chama, usaliti wakati na baada ya uchaguzi mkuu
hali iliyopelekea CCM kupoteza kata ya kidatu viongozi hao wakiongozwa
na mwenyekiti wa CCM kata ya kidatu Ndugu Mangungu Alex waliomba
kujiuzulu nafasi zao zote za uongozi ndani ya chama, kuomba radhi
wanachama wa CCM na kuahidi kubaki kuwa wanachama waaminifu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Akisisitiza
uamuzi huo katika kikao hicho cha ndani Ndugu Polepole alisema Kama
mtumishi wetu namba moja kwenye Chama na Serikali yetu Ndugu John Pombe
Joseph Magufuli anajua kuwa cheo ni dhamana, wewe mwingine unapata wapi
nguvu ya kutumia cheo kwa faida yako
Akitoa
neno la kuhitimisha Ndugu H.H. Polepole amesema Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kinafanya mageuzi makubwa ya kurejesha chama kwa wanachama,
kusimamia rasilimali za chama zitumike kwa manufaa ya chama, kujenga
misingi imara ya utoaji haki ndani ya chama pamoja na kuhakikisha katika
chaguzi zinazoendela CCM inapata viongozi wenye sifa “Haipaswi wakati
wowote kugeuza Chama hiki kuwa chama cha viongozi, Chama hiki tangu
awali msingi wa kuanzishwa kwake ni kuwa kiwe chama cha wanachama na
kinachoshughulika na shida za watu
Pia
Ndugu Polepole amempokea na kuagiza uongozi wa ngazi ya tawi kumpokea
na kumpa mafunzo ya Itikadi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) aliyekuwa
mgombea udiwani na Mwenyekiti wa ACT kata Kidatu Ndugu Deodatus Makolo
ambaye leo amejivua nafasi zake zote za uongozi katika chama hicho na
kujiunga na CCM.
Ndugu
H.H. Polepole yupo ziarani Mkoa wa Morogoro, kukagua na kujionea zoezi
la uchaguzi wa ndani ya Chama ngazi ya msingi unaoendelea, kipindi hichi
ambacho CCM inafanya mageuzi makubwa ya kiuongozi, kimuundo na
kiutendaji. Ziara hii ni muendelezo wa ziara za kichama na vikao vya
ndani vyenye lengo la kutoa hamasa, kuvumisha umuhimu wa Mageuzi ya
Chama, kuimarisha Chama na kutatua kero za wanachama.
Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Julai 28, 2017.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇