*AFUNGA KAMBI YA MAFUNZO KWA VIJANA KUTOKA VYUO KUMI VYA MJINI DODOMA
* VIJANA WAAHIDI KUMUUNGA MKONO JPM
Wanafunzi kutoka vyuo kumi vya Mjini Dodoma wamemaliza Kambi ya mafunzo ya siku tatu yaliyotolewa kwa lengo la kuwaongezea Ufahamu juu ya Chama Cha Mapinduzi na Mambo mbalimbali yanayoendela hapa nchini.
Mafunzo hayo yaliyofunguliwa 23/06/2017 na Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole na kufungwa 25/06/2017 na Katibu wa NEC siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela Lubinga yalihusisha wajumbe 551 wa Vyuo na Vyuo Vikuu vilivyopo katika Mkoa wa Dodoma.
Akizungumza wakati wakati wa Kambi/Mafunzo hayo Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, alisema Serikali ya awamu ya tano imejizatiti kikamilifu kupambana na wezi wa mali za umma.
"Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli imejipanga katika kuzuia mianya yote ya rushwa, nasisitiza kuwa hakuna mwizi atakayesalia katika ujenzi wa CCM Mpya na Tanzania mpya", alisema Kanali Lubinga
Pia akizungumza baada ya kufungwa mafunzo hayo Kaimu Katibu wa Idara ya Vyuo na vyuo vikuu UVCCM Ndg. Daniel Zenda alisema kambi imeisha salama na vijana wameyapokea vizuri mafunzo hayo.
"Tunamshukuru Mungu tumemaliza salama kambi/ mafunzo yetu na vijana wameyapokea vizuri na kuahidi kuyafanyia kazi yale yote waliyofundishwa sambamba na kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli kwa yale yote anayoyafanya", alisema Kaimu Katibu wa Vyuo na Vyuo Vikuu Daniel Zenda.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo hayo waliwataka wawe wazalendo kwa nchi yetu sambamba na kumuunga mkono Rais Magufuli kwa yale anayoyafanya ya kuwatetea wananchi wa Tanzania hususani Maskini na wanyonge. Dhamira na hatua anazochukua tunaziona kwa Vitendo ni dhahiri na ni shairi. "Maana Uzalendo ni Vitendo"
Wakati huo huo baada ya kumaliza mafunzo hayo Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela Lupinga aliweka Jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa Ofisi ya Vyuo na Vyuo Vikuu Tawi la Hombolo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇