LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 2, 2017

MAONI: RAIS DK. MAGUFULI ANAVYOLIHUISHA AZIMIO LA ARUSHA

Azimio la Arusha ni tamko rasmi la kisiasa lililokusiwa kuongoza Tanzania  Kijamaa kadiri ya kauli ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Tamko hilo lilitolewa mjini Arusha na lilipitishwa tarehe 26-29 January 1967.

Tamko la Arusha lina sehemu tano, Yaani Itikadi ya Chama cha TANU, Siasa ya Ujamaa, Siasa ya kujitegeea, Uanachama wa TANU na Azimio la Arusha.

Kiini chake ni hiki, Tumeonewa kiasi chakutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha na unyonge wetu ndio umetufanya tuonewe.

Lengo kuu la Azimio la Arusha ni kupinga unyonyaji, ubaguzi ili kuleta usawa ndani ya jamii.

Hili lilikuwa ni azimio lenye misingi ya utu, na lengo kubwa la AZIMIO LA ARUSHA ni kujitegemea, kiuchumi na si kisiasa peke yake na hasa kuwaondoa Waafrika katika mawazo ya kitumwa, kama Bob Marley alivyoimba, Emancipate yourself from mental slavery.

Kitendo cha JPM kufuta posho, safari za nje, wakubwa kupunguzwa nguvu ya ubabe, Mali za watumishi wa umma kuhakikiwa, kuzuia kusafirishwa kwa wanyama hai na madini nje ya nchi, kuchunguzwa kwa mchanga wa madini, kutoa elimu bure yote haya ni matendo yanayoendana na misingi ya Azimio lililotaka kuondoa ubaguzi, kuondoa matabaka ndani ya jamii, kudumisha utu, kuondoa unyonyaji ili tuweze kujitegemea kiuchumi.

Tumeanza kuheshimiana sasa. Ule msemo wa laki si pesa umekufa kabisa, zile kauli za unanijua Mimi nani hakuna tena. Haki ipo kwa wote ndani ya jamii.

Hauwezi kuyafanya hayo bila ya kuwa na uzalendo kama alionao Rais Magufuli. Naona kila dalili Rais Magufuli akiturudisha kulienzi na kulidumisha Azimio la Arusha lililoasisiwa na Mwalimu Nyerere

Na Emmanuel J. Shilatu
01/06/2017
0767488622 

3 comments:

  1. Hi! I just wanted to ask if you evrr have any trouble with hackers?

    My last blog (wordpress) was hacked and I ended up losing many months of hard
    workk due to noo dat backup. Do you have any solutions to stopp
    hackers?

    ReplyDelete
  2. This is really interesting, You're a very skilled blogger.
    I have joined your rss feed and look forward to seeking
    more off your fantastic post. Also, I have shared your site
    in my social networks!

    ReplyDelete
  3. Hello, of ourse this post is in fsct nice and I have learned lot of things from
    it concerning blogging. thanks.

    ReplyDelete

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages