Bajeti
Mpya ya Serikali ya mwaka 2017/2018 ndiyo Bajeti ya pili tangu Serikali ya
Awamu ya Tano iingie madarakani chini ya Uongozi mahiri wa Mhe. Rais Dr. John Joseph
Pombe Magufuli, bajeti hii iliyopitishwa kwa asilimia 73 ya wabunge wote wa
Bunge la Jamuhuri 20/07/2017 imeonyesha nia ya dhati kabisa katika kuyafikia
malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 ambayo ni kuufikia Uchumi wa Kati
wenye sifa kubwa ya Viwanda.
Kilichogusiwa
katika bajeti hii ni kuongeza kasi ya kukua kwa Uchumi kwa ujumla, kusimamia Rasilimali
za Taifa na kuthibiti Mapato yatokanayo na rasilimali hizo, kuimarisha nidhamu
ya watumishi wa Umma na kuhakikisha tunakuwa na Miundombinu safi na salama ili
kujihakikishia wawekezaji wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi.
Bajeti
hii pia imehakikisha kuwa tunanufaika vilivyo na Rasimali zetu za Madini na Gesi,
tunakuza zaidi Sekta ya watu binafsi, tunakuza hali ya kilimo chetu kuwa chenye
tija na ufanisi zaidi kuliko hapo awali, kufanya juhudi zaidi za kuongeza idadi
ya watalii hapa nchini kwa kuvitangaza zaidi vivutio vyetu, kuongeza ufanisi
katika Sekta nzima ya Elimu, Serikali imejidhatiti kutoa Elimu bora na yenye
tija kwa maendeleo ya nchi yetu, pia Serikali imeamua kuondoa Urasimu usiokuwa
na maana sehemu zote za kazi na kupambana na Rushwa kwa vitendo kama ambavyo
juhudi zimeshaanza kufanyika.
Sehemu
zilizotiliwa mkazo katika Bajeti hii ni pamoja na kuongeza kasi ya Ukuaji wa Uchumi,
kuongeza kasi ya ukuaji wa Sekta ya viwanda kama ambavyo Rais ameweza
kusisitiza. Kukuza Ueledi katika kazi miongoni mwa wanataaluma na kutengeneza
mazingira rafiki sana kwa biashara mbalimbali na viwanda pia.
FURSA MBALIMBALI ZA VIJANA ZILIZOPO
KATIKA BAJETI MPYA 2017/2018
KUONDOLEWA KWA KODI YA ONGEZEKO LA
THAMANI KATIKA SHUGHULI ZA USAFIRISHAJI NA FORODHA
Mwaka
jana kodi hii ililalamikiwa sana mpaka baadhi ya watu walidai imepunguza idadi
ya watumiaji wa Bandari yetu, ni jambo la kushukuru kuona kwamba Serikali
ilisikia kilio chetu na kulifanyia kazi na sasa hakuna VAT za watoa huduma Bandarini.
Tulishuhudia wateja wetu wakubwa wa bandari yetu kama DRC, ZAMBIA, MALAWI,
UGANDA, BURUNDI na RWANDA wakitumia bandari zingine kama Mombasa, Beira hadi
Pretoria, sasa kikwazo hakipo tena. Hivyo tunawasihi vijana wachangamkie fursa
hii adhimu kwa vile barabara zetu bado ni bora sana, na kijiografia sisi ni
karibu sana na wao, tujitahidi kufanya kazi kwa bidii tuwarudishe wote na
kuongeza zaidi.
KUFUTWA KWA KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI
(VAT) KWENYE BIDHAA ZA MITAJI (CAPITAL GOODS)
Hili
ni jambo la heri ambalo linafaa vijana wote kulijua vizuri. Kodi hii ndiyo ilikuwa
inafanya gharama za ununuzi wa mashine za kutengenezea bidhaa mbalimbali kuwa
ghali sana, kwa sasa ukiagiza mashine za kuzalishia bidhaa zingine hutotozwa
VAT wala Import duty, hii inahamasisha sana watu kununua mashine na kufungua viwanda
vidogo vidogo, hima vijana tuanze kufungua viwanda, na habari njema ni kwamba
kuna taasisi nyingi za kifedha zinazotoa mikopo rahisi kabisa kwa wale ambao wamedhamiria
kwa dhati kabisa kuanzisha biashara. Kadharika tunayo Mifuko mbalimbali ya Maendeleo
ya Jamii kutoka Serikalini inayotoa Mikopo na Ruzuku kwa makundi mbalimbali
hususani vijana.
KUFUTWA KWA KODI YA ROAD LICENCE/ MOTOR
VEHICLE
Kodi
ya gari kutokana na matumizi ya barabara ilikuwa inakusanywa moja kwa moja na TRA
kutoka kwa watumiaji wa magari, hali hii ilipelekea kuifanya kodi hii iwe
inamuumiza kwa kiasi kikubwa mlipaji kutokana na ukubwa wa gharama na kodi hiyo
kushindwa kubaini ni magari gani yanatumia barabara na yapi hayatumii, pia kodi
hii iliifanya Serikali kupoteza mapato mengi kutokana na urahisi wa kuikwepa. Kitendo
cha Serikali kuihamishia kodi hii kwenye mafuta kitaondoa maumivu ya ulipaji, kitafanya
Serikali ikusanye mapato yake Stahiki na kwa kuwa itakusanywa kwa magari
yanayotembea tu itaongeza uhalali kwa walengwa wote.
KUFUTWA VAT –KODI YA ONGEZEKO LA
THAMANI KWA MASHINE ZA KUTOTOLESHA KUKU NA CHAKULA CHA KUKU.
Hii
nayo ni nafuu kubwa kwa vijana kwa kuwa zile incubators hazitakuwa ghali tena,
ilikuwa aibu kwa nchi kubwa kama Tanzania kuingiza mayai na kuku kutoka nchi
jirani kwa sababu ya bei kuwa rahisi, kuondolewa kwa kodi hii kutaleta unafuu
mkuwa katika kuendesha biashara ya kuku. Jambo hili litapunguza gharama kubwa
za kuzalisha kuku na mayai pia, hii iwe fursa ya kuweza kuuza kuku na mayai
kwenye nchi za jirani visiwani hata mbali kabisa ya maeneo yetu, iwe fursa
kwetu kuongeza wigo wa ushindani wa kimataifa huku tukisaidiwa na mabalozi wetu
kujua fursa mbalimbali zilizopo nje ya nchi.
KUPUNGUZWA KWA KODI YA FAIDA KWENYE
SEKTA YA KUTENGENEZA MATREKTA, KUUNGANISHIA MAGARI NA BOTI ZA UVUVI
Kwa
kawaida Sekta hii ilitakiwa ilipe 30% ya faida yao kama kodi, sasa kwa kuwa Serikali
imeamua kunufaisha kilimo na uvuvi imeamua kwenda mbele zaidi na kupunguza kodi
hii kutoka 30% mpaka 10%, kwa kufanya hivi Serikali imewapa ahueni kubwa wale
wanojihusisha na uundwaji wa magari, maboti, na pia matrekta. Hii yote
imefanywa ili ndoto ya kuwa na viwanda vya kutosha itimie, wawekezaji wengi wa
ndani na nje hukimbilia sehemu ambazo hazina kodi kubwa kama hapa kwetu, sasa
vijana yafaa kuchangamkia fursa hii kwa kuleta wawekezaji ambao watawekeza hapa
na kuuza ndani na nje ya nchi yetu kutokana na unafuu mkubwa wa kodi uliopo
ndani ya nchi ukilinganisha na majirani zetu.
KUFUTWA KWA KODI YA VIFAA VYA WALEMAVU.
Vifaa
vya watu wenye ulemavu vitapatikana kwa nafuu hivyo kuwezesha walemavu wengi
kuvipata na kuwasaidia katika shughuli zao za kila siku ikiwemo utafutaji wa
riziki. Pia itasaidia kupunguza utegemezi wa ndugu, jamaa na marafiki hivyo
kufanya Nguvukazi ya Taifa kuwa hai katika shughuli za kimaendeleo.
SERIKALI IMEAMUA KWA DHATI KABISA
KULINDA VIWANDA VYA NDANI KWA KUFANYA YAFUATAYO;
Juisi
inazotengenezwa hapa nchini imepunguziwa kodi kutoka asilimia 9.5 mpaka asilimia
9, Wine zinazotengenezwa hapa nchini zimepunguziwa kodi, Vinywaji vikali navyo
vimekuwa na kodi ndogo kuliko vinavyotoka nje, Sigara zinazotengenezwa ndani
zinatozwa kodi kidogo ukilinganisha za zile za nje. Kodi za mazao zimepunguzwa sana,
kwa mazao ya biashara, kodi imepungua kutoka asilimia 5 mpaka asilimia 3, vile
vile kodi za mazao ya chakula zimepungua kutoka asilimia 5 mpaka asilimia 2,
yote hii imefanyika ili sisi vijana tukalime na tuwe washindani wakubwa wenzetu
kwenye masoko ya kimataifa kwa kuwa mazao yetu yatakuwa na bei rahisi sana.
SERIKALI SIKIVU YA CHAMA CHA MAPINDUZI
HAIKUISHIA HAPO BALI IMEENDELEA KUONDOA KODI KERO ZOTE KAMA IFUATAVYO;
Imeondoa
TOZO zote zilizokuwa kwenye mbolea wakati wa kununua ambazo ni kama zifuatavyo,
TBS- Tanzania Bureua of standards, TAEC - Tanzania Atomic Energy Commission WMA
–Weight and Measures Authority. Kuondoa TOZO zote hizi kwenye mbolea kunaifanya
mbolea kuwa na bei rahisi sana kiasi cha kwamba kila mkulima ataweza kumudu
gharama kidogo za mbolea maaana yake atapata mazao mengi zaidi ukilinganisha na
kama mbolea isingetumika kabisa, Rai ni kwa vijana kuliona hili na
kulichangamkia haraka bila kupoteza wakati, kama fedha ama mtaji ni shida basi
ni vyema kutumia Mifuko ya Maendeleo ya Jamii na taasisi zingine za kifedha
kukopa na kuchukua hatua ya kufanya uzalishaji.
Imeondoa
TOZO zote za viwango vya ubora na ukaguzi zilizokuwa zitkitozwa na TBS –
Tanzania bureau of Standards kwenye mazao kama pamba, chai, korosho na kahawa.
Kama ambavyo Mhe Rais aliahidi akiwa kwenye kampeni kule Bukoba kwamba watu wataenda
kuuza kahawa Uganda, hakika katimiza Ahadi hizo kwa sasa tozo zote
zimeondolewa, sasa kilimo kina tija tena. Hima vijana wenzetu kama tunahitaji
mali basi zinapatikana mashambani.
TOZO
za nyumba za kulala wageni, zile kodi za service levy kwenye guest house
zimefutwa rasmi, so kwa wale wenye ndoto za kumiliki nyumba za kulala wageni
hii sekta ni muhimu kwa kuwa imekuwa haina gharama tena, Rai yetu ni ile ile
kwamba Serikali imeandaa mazingira mazuri kwa sisi, ni fursa ya kuchangamkia
mapema ili tuweze kustawi, si vyema waje watu kutoka nje kuja kuchuma haya
matunda wakati sisi tumelala na kulalamika kila uchwao.
TOZO
za kupata kibali cha kuchinja wanyama zimefutwa, na tozo za kusafirisha wanyama
nazo zimefutwa hii yote imefanyika ili kupunguza gharama za maisha ya sisi sote
na vilevile kuhamasisha vijana kujihusisha na biashara hizi. Kwa wale ndugu
zetu wenye mifugo mara nyingi wakipeleka mifugo yao kwenye minada hutozwa fedha
za mnada kwa kuwepo kwenye soko husika. Sasa Mhe. Rais kafuta hii tozo
kupunguza gharama zisizo na msingi na kufanya maisha yawe rahisi zaidi lakini
cha zaidi ni kurahisisha ufanyaji wa hii biashara, kwa maana hiyo vijana
wanahamasishwa kuingia na kufanya hii biashara.
Katika
kulinda Viwanda vyetu vya ndani Mhe Rais kapandisha TOZO mbalimbali za bidhaa
ambazo zinapatikana kwa wingi hapa nchini kwetu lakini bado watu wanaziagiza
toka nje. Bidhaa kama za makaratasi, Sukari kwa ajili ya kulisha viwanda, Bidhaa
za chuma, Bidhaa za gypsum, Mawese na bidhaa za Alminium (kaongeza kodi kwa
zile za nje na kupunguza kodi kwa zile zinazozalishwa ndani).
Mgawanyo
wa Bajeti yetu ni kama ifuatavyo; 61% mapato ya ndani ya kawaida, 24% mikopo ya
ndani yenye riba nafuu na ya kibiashara vilevile, 13% Ni mikopo ya nje na
misaada ya wahisani na 2% Hizi ni tozo kutoka Serikali za mitaa.
Tunaweza
kuona ni jinsi gani tulivyopunguza utegemezi wa wahisani, sasa ni dhahiri kabisa
kuwa tunaelekea sehemu nzuri zaidi ya kutotegemea misaada kabisa, kwa mfano
mwaka wa fedha uliopita hatukupata fedha za kutosha kutoka kwa wahisani lakini
tuliweza kuendesha Serikali vizuri na miradi mikubwa ikaendelea kama kawaida.
Jambo
la kujivunia ni kwamba ukiangalia matumizi ya Bajeti hii ni kwamba takribani
asilimia 62 ya matumizi ya Serikali ni kwa ajili ya Maendeleo mbalimbali ya
nchi kama vile; miradi ya Barabara, Vivuko, Meli, Ndege, Maji, Umeme, Reli, na
vingine vingi. Ni asilimia 38 tu ndio inaenda kwenye mtumizi ya kawaida ambayo
ni pamoja na Mishahara, Posho, Vitafunwa, Safari, per diem, Stationeries na
vingine vidogo vidogo.
Hii ni hatua kubwa kuwahi kufikiwa kwa kuwa hapo miaka
ya nyuma tulikuwa hatuwezi kufanya mambo ya maendeleo bila kukopa, kiasi chote
tulichokuwa tukikusanya kilikuwa kinaenda kufanya matumizi ya kawaida lakini
kwa sasa hali imebadilika kabisa ni vyema sasa vijana wakaona manufaa ya
mabadiliko haya kwa mfano;
Mradi Mkubwa wa Reli ya kati (Standard Gauge) unakuja na fursa nyingi sana, kuanzia mama ntilie, wasafirishaji, wenye makampuni ya ujenzi, wajenzi wa nyumba, watu wa Clearing and Forwading, mahoteli na vingine vingi sana, madereva, Mafundi. Uwepo wa Reli ya kati utawezesha usafiri wa haraka na nafuu, Mfano Samaki zinazovuliwa Mwanza zitaliwa Dar es Salaam kwa wakati zikiwa fresh, mazao ya mbogamboga kutoka kutoka Morogoro yaliyokuwa yakiozea njiani yatafika kwa wakati na kwa urahisi na Bei za bidhaa zitashuka kutokana na kushuka kwa gharama za usafirishaji. Hizi zote ni fursa zetu vijana kuzalisha mazao mbalimbali na kupata faida kubwa.
Mradi Mkubwa wa Reli ya kati (Standard Gauge) unakuja na fursa nyingi sana, kuanzia mama ntilie, wasafirishaji, wenye makampuni ya ujenzi, wajenzi wa nyumba, watu wa Clearing and Forwading, mahoteli na vingine vingi sana, madereva, Mafundi. Uwepo wa Reli ya kati utawezesha usafiri wa haraka na nafuu, Mfano Samaki zinazovuliwa Mwanza zitaliwa Dar es Salaam kwa wakati zikiwa fresh, mazao ya mbogamboga kutoka kutoka Morogoro yaliyokuwa yakiozea njiani yatafika kwa wakati na kwa urahisi na Bei za bidhaa zitashuka kutokana na kushuka kwa gharama za usafirishaji. Hizi zote ni fursa zetu vijana kuzalisha mazao mbalimbali na kupata faida kubwa.
Mradi mwingine mkubwa ni ule wa bomba
la kutoka Uganda mpaka Tanga. Biashara ya Mafuta ni
biashara adimu na muhimu duniani kote. Mafuta ni uchumi, mafuta ni fedha.
Upatikanaji wa Petrol, Mafuta ya Ndege na Diesel utasaidia kuimarisha uchumi wa
nchi. Kadharika vijana wengi watapata ajira kwenye maeneo hayo na kutakuwa na
uingizaji wa fedha za kigeni. Vilevile itanufaisha watu wanaojihusisha na masuala
ya usafirishaji, wauza vyakula, watu wa Clearing and Forwarding, wamiliki wa Mahoteli,
wenye magari ya kukodisha, malazi na vingine vingi.
Ununuzi wa ndege nyingine. Pato
la Taifa litaongezeka kupitia ulipaji wa kodi, watalii wataongezeka, vijana
wengi watapata ajira kwenye nafasi mbalimbali kama vile urubani, uhudumu wa
ndani, uuzaji wa vyakula ndani ya ndege, uuzaji wa mafuta ya ndege. Mpaka sasa
Serikali imekwisha nunua ndege mbili zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja
ambapo ndege hizo zilianza kutoa huduma tangu October 2016. Huku moja nyingine
inategemewa kuwasili Julai 2017, mbili zinategemewa kuwasili June 2018 na ya
mwisho ambayo itakuwa ni ya masafa marefu inategemewa kuwasili Julai 2018.
Kuimarisha Sekta ya Usafiri wa Anga pia kunachochea Maendeleo ya Biashara
kutokana na urahisi wa kusafirisha bidhaa ndani na nje ya nchi na kuondokana na
upotevu wa muda kwa wafanyabiashara.
Ujenzi wa kiwanda kikubwa cha Chuma
kule Liganga na Mchuchuma Njombe. Hii ni fursa adhimu
sana kwa nchi yetu vijana wakae chonjo kwa kuwa biashara ya usafirishaji,
uuzaji chakula na zingine nyingi zitatokea hapa. Nchi nyingi zilizoendelea kama
vile China na Ulaya hutumia madini haya kwenye viwanda vikubwa ili kupunguza
gharama za uzalishaji kwenye viwanda vyao. Upatikanaji wa madini haya Tanzania
utasaidia kuwa na uhakika wa uzalishaji na kuongeza ajira kwa vijana wengi kwa
sababu wawekezaji wengi watavutiwa kuanzisha viwanda nchini.
Ujenzi wa LNG-PLANT, Liquified Natural
Gas (Mitambo ya kusindikia Gesi kimiminika) Lindi. Gesi ni moja ya
vyanzo vinavyozalisha umeme. Gesi imesaidia kurahisisha uzalishaji wa Umeme wa
Grid ya Taifa ambao pia unasaidia kwa kiasi kikubwa kwenye viwanda. kuanza kwa ujenzi wa Mradi huu kutakuwa na
manufaa makubwa sana kwetu kama watanzania, Ajira nyingi zitazaliwa humu,
vilevile ujenzi wa kiwanda cha mbolea inayotengenezwa kwa kutumia gesi nao
utaanza, kwa hiyo wale vijana ambao ni wahandisi wakae mkao wa kula, wamiliki
wa magari ya usafirishaji, wale wakulima wajiandae kupata mbolea ya bei rahisi
zaidi. Taifa litajiingizia fedha za kigeni kwa kuuza gesi
nje ya nchi, kadharika itarahisisha matumizi ya nyumbani yanayotokana na umeme na
hatimaye kuongeza ubora wa maisha.
Kupunguza kodi kwenye Masoko ya Matunda
ndani. Uzalishaji wa mazao kwa wakulima sasa utakuwa sio wa
mashaka, maendeleo ya kujitegemea na kujiajiri na maendeleo ya viwanda vya
ndani yatakuwa kwa kasi, itaongeza hamasa ya uzalishaji wa matunda kwa wakulima
kutokana na ongezeko la soko la na pato lao hivyo kupelekea kuongezeka kwa
ajira, ukuaji wa sekta ya kilimo pamoja na kuongezeka kwa pato la Taifa
kadharika iatwezesha kukua kwa viwanda vinavyotengeneza Juisi. Ipo haja yetu
kuongeza ubora kwenye bidhaa za ndani ili kupambana kikamilifu na ushindani
mkubwa utakaoibuka.
Usambazaji wa Umeme Vijijini kupitia Mradi
wa REA. Kwa
mujibu wa Bajeti hii mpaka sasa wateja (watanzania vijijini) 146,831 sawa na
asilimia 58.7 ya lengo wameunganishwa wakati hatua za makusudi zinaendelea kwa
ajili ya kuwafikia wateja wote waliolengwa. Kwanza gharama za ufikishaji wa
Umeme huu majumbani ni nafuu takribani TShs 27,000 hutumika kulipia. Hii ni
fursa kwetu vijana kwa sababu umeme unapunguza gharama za mafuta yaliyokuwa
yakitumika kuwashia mwanga na kwenye majiko ya kupikia. Sasa kazi za ajira
zitafanyika huko huko vijijini na sio kutegemea mijini, uimarishwaji wa mawasiliano
kwa wafanyabiashara na uimarishaji wa biashara za vinywaji kutokana na urahisi
wa kutumia friji. Ni wakati wa kuimarisha Viwanda vidogo vidogo kama vile
viwanda vya uchomeleaji, wakata vyuma, Viwanda vya Useremala, Mashine ndogo za
kufyatua matofali, saluni, ujenzi, usindikaji na vyakula ili kunufaika
kikamilifu na fursa hii.
Urasimishwaji wa Machinga. Kutambuliwa
kwa wafanyabiashara wadogowadogo kisheria kutaisaidia wao kupata haki za
kisheria na faida za kibiashara kama kuweza kuongeza mitaji yao kupitia mikopo
ya kati na mikubwa. Hii itapelekea kutengeneza wafanyabiashara wakubwa na wengi
nchini, kupata nafasi ya kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kama NSSF, NHIF
nk. Itasaidia Serikali kuongeza wigo wa mapato yatakayotokana na malipo ya Leseni
ya Biashara, Ushuru wa Soko pamoja na Ushuru wa Bidhaa.
IMETOLEWA NA IDARA YA UHAMASISHAJI NA
CHIPUKIZI
UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇