Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, akiongea na Mahakimu na Watumishi wengine wa Mahakama (hawapo pichani), katika maongezi yake na Watumishi hao Mhe. Jaji Prof. Juma amewataka na kuwasisitiza Watumishi hao kufanya kazi kwa kuzingatia Maadili ikiwa ni pamoja na kuwa na lugha nzuri kwa Wateja/Wananchi wanaowahudumia. kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha na kushoto ni Mhe. Rumisha, Naibu Msajili-Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha. |
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Juma akisamiliana na Watumishi wa Mahakama, Kanda ya
Arusha alipowasili katika viwanja vya Mahakama Kuu-Arusha kukamilisha
ziara yake ya siku mbili mkoani humo.
Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi,
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,Mhe. Kamugisha akimsomea taarifa ya hali
ya utendaji kazi wa Mahakama katika mkoa huo. Lengo la ziara ya Mhe.
Kaimu Jaji Mkuu katika Kanda hiyo ni kujifunza na kuona hali halisi ya
mazingira ya kazi na utekelezaji wa majukumu.
Naibu Msajili, Mahakama Kuu,
Kanda ya Arusha, Mhe. Rumisha (wa kwanza kulia) akimuonesha Mhe. Kaimu
Jaji Mkuu, moja ya kumbi za Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha pindi
alipokuwa akikagua ofisi mbalimbali za Mahakama ya Mkoa na Mahakama Kuu
katika Kanda hiyo.
Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Juma
akiwa katika Kompyuta Mpakato akikagua Mfumo wa Kuratibu takwimu za
Mashauri kwa njia ya Kielektroniki (JSDS) kuhakikisha kama inafanya kazi
ipasavyo, pembeni ni Afisa TEHAMA, Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha, Bw.
Athuman
Mahakimu na Watumishi wengine wa Mahakama wakimsikiliza Mhe. Kaimu Jaji Mkuu alipokuwa akizungumza nao.
Mtendaji, Mahakama Kuu-Arusha,
Bw. Edward Mbara akiwasilisha taarifa ya hali ya utendaji kazi wa
Mahakama katika mkoa huo mbele Mhe. Kaimu Jaji Mkuu na Watumishi wa
Mahakama, katika taarifa yake Bw. Mbara alikiri kuwa Kanda ya Arusha
inakabiliwa na changamoto kubwa ya miundombinu chakavu ya majengo ya
Mahakama n.k (Picha na Mary Gwera,Arusha)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇