Mwandishi akitokwa damu mkononi |
Na Mwandishi Wetu
BAADHI ya waandishi wa habari na wanachama wa CUF wamejeruhiwa baada ya watu wanane, waliokuwa wamevalia ninja na kuvamia mkutano wa wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF), mabibo jijini Dar es Salaam.
Vurugu hizo zimetokea leo, wakati wanachama wa CUF walipokuwa kwenye mkutano huo na waandishi wa habari katika Hoteli ya Viva jijini Dar Es Salaam.
Vurugi hizo zilizua taharuki kubwa kwa waandishi wa habari na wakazi wa eneo hilo ambapo walifanikiwa kumkamata mmoja wa watuhumiwa hao na kumkata mguu wa upande wa kulia.
Baadhi ya mashuhuda wanasema watu wasiojulikana walifika katika eneo hilo wakiwa wamefunika nyuso zao na vitambaa huku wakitumia silaha za jadi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na taarifa zaidi atatujuza baada ya kufika eneo la tukio
PICHA YA VIDEO>BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇