Masanja Mabula -Pemba
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema imechoshwa na vitendo vya hujuma vinavyofanywa na watu wasioitakia mema Zanzibar
na kuahidi kushusha kikosi kazi cha askari kutoka Jeshi la Polisi Makao
Makauu ili wafanye uchunguzi na wahusika waweze kupatikana na
kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Imesema vitendo hivyo vinafanywa
na watu kwa makusudi vinarudisha nyuma maendeleo ya nchi na wananchi
wake pamoja na kuhatarisha usalama , amani na utulivu wa nchi.
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili Mohammed Aboud
Mohammed wakati akizungumza na wananchi katika kitalu cha miti ya
matunda na misitu cha wanakikundi wa kaya maskini kilichomwa moto huko Nyali Mtambwe Wilaya ya Wete usiku wa kuamkia Jumapili.
Amesema
Serikali itawasiliana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania pamoja na
Kamishna wa Polisi Zanzibar haraka iwezekanavyo ili kikosi hicho kifike
na kuanza kazi ya uchunguzi dhidi ya wahalifu wanaoendesha vitendo vya hujuma hizo.
Waziri
Aboud amewataka wananchi kushirikiana na Kikosi hicho kwa kutoa taarifa
sahihi ambazo zitafanikisha kuwabaini wahusika na vitendo hivyo na
hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kufikishwa
mahakamani.
“Kikosi
kazi kutoka Jeshi la Polisi makao makuu kitatumwa haraka iwezekanavyo
kufanya uchunguzi wa kina juu wa wahusika wa matukio haya , Serikali
imechoshwa na hujuma za kila siku kwa sasa tumeamua kuvikomesha
tunawaomba wananchi watoe ushirikiano ”alifahamisha.
Aidha
Waziri Aboud amefahamisha kwamba katika hilo Serikali itakusudia
kuendesha kura ya siri katika shehia hiyo ambayo itasaidia kuwaweka
bayana wahusika na wanajihusika na vitendo vya kuhujumu mali za wananchi
wasio kuwa na hatia .
Mapema
Mkuu wa Wilaya ya Wete Rashid Hadidi Rashid amemweleza Waziri kuwa
tayari Serikali ya Wilaya inazo taarifa za awali juu ya wahusika wa
hujuma hizo na kwamba ameviagisa vikosi vya ulinzi kuhakikisha
wanawakamata kwa ajili ya upelelezi .
Amesema kuwa kitalu hicho ambacho kinasimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii nchini TASAF , ni moja ya miradi iliyoibuliwa na wananchi wenyewe
ambao walikusudia kuipanda sehemu za wazi ili kurejesha uhalisia wa
maeneo hayo .
Akitoa
utafafanuzi , Afisa Kutoka Idara ya Misitu Pemba Assaa Sharif Ngwali
amesema ndani ya kitalu hicho tayari miti mbali mbali ikiwemo miembe ,
Mifenesi , Mitondoo na misaji ambapo malengo ya baadaye ni kuotesha miti
22,000.
Aidha
hujuma hizo pia zzilizofanywa na watu wasiojulikana wamekata kata
migomba 40 ya Shufaa Assa Muombwa pamoja na shamba la Mihogo la Khamis Oma Kibano lenye ukubwa wa ekari ambapo mashsina 397 yameng’olewa
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇