Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika benchi la kibanda cha kupigia kiwi (Shoe Shine) pamoja na wakazi
wengine wa Chato katika eneo maarufu kama Stendi za zamani Chato mkoani
Geita. Kibanda hicho cha Kiwi ndicho Rais Dkt. Magufuli alichokuwa
akisafishiwa viatu vyake kabla ya kuwa Rais, pia ni sehemu ambayo
alikuwa akipenda kukaa na kubadilishana mawazo na wakazi wa Chato
wakati akiwa mapumzikoni kipindi cha Nyuma.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akifurahia
pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato mkoani Geita. Shule hiyo ya
Msingi Chato ndiyo Rais Dkt. Magufuli alisoma kuanzia darasa la kwanza
mpaka Darasa la Saba. Rais Dkt. Magufuli amewaasa Wanafunzi hao kusoma
kwa bidii kwasababu yeye pia alisoma shuleni hapo. Picha na Mpigapicha
Maalum.
TAARIFA KAMILI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 9 Januari, 2017 amefanya ziara ya kushtukiza katika Shule ya Msingi Chato,ambapo ndipo aliposoma kuanzia darasa la kwanza hadi la saba na kuzungumza na walimu na wanafunzi wa shule hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 9 Januari, 2017 amefanya ziara ya kushtukiza katika Shule ya Msingi Chato,ambapo ndipo aliposoma kuanzia darasa la kwanza hadi la saba na kuzungumza na walimu na wanafunzi wa shule hiyo.
Rais Dkt
Magufuli ameahidi kujenga madarasa matatu na ofisi moja ya walimu katika
Shule hiyo kufuatia ombi la Walimu kuwa shule hiyo inakabiliwa na uhaba
wa vyumba vya madarasa ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi wanaosoma
shuleni hapo.
Aidha
Dkt.Magufuli amewaasa wanafunzi kutilia mkazo masomo ili waweze
kufaulu na kuwataka walimu kuhakikisha wanatumia vyema fedha
zinazotolewa na Serikali kila mwezi katika kutoa elimu bila malipo
na pasiwe na wanafunzi hewa kama ilivyo kwa baadhi ya shule ambazo
zimegundulika kuwa na wanafunzi hewa katika uhakiki uliofanywa na
serikali.
Kwa
upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chato, Bwana Mwita Chacha
amemshukuru Rais Dkt.Magufuli kwa msaada aliowapatia katika kukabiliana
na uhaba wa madarasa uliokuwa unaikumba shule hiyo, pia kuitembelea
Shule yao jambo ambalo limewatia moyo walimu na wanafunzi shuleni hapo.
Rais
Magufuli pia ametembelea eneo la Stand ya zamani na kuzungumza na baadhi
ya wananchi waliokuwepo eneo hilo na kutoa msaada kwa kikundi cha
wasafisha viatu ili kuongeza mtaji wa biashara yao.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato, Geita.
9 Januari, 2017
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇