Rais
mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akiwatunuku
wahitimu wa kozi mbalimbali katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Kampala
cha jijini Dar es Salaam kwenye sherehe za mahafali.
Baadhi ya waadhiri wa chuo hicho wakiwa kwenye mahafali hayo.
Rais
mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na
mgeni rasmi katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Kampala cha jijini Dar es
Salaam akiteta jambo na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Muhammad
Ndaula katika mahafali hayo yaliyofanyika jana.
Baadhi ya wahitimu wa ngazi ya digree kozi ya afya wakila kiapo cha kuhitimu fani hiyo.
Sehemu ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
Sehemu ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
Sehemu ya wakufunzi na wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kampala wakiwa kwenye mahafali.
Mahafali yakiendelea
Msafara wa mahafali ukiongozwa na Rais msaafu wa Awamu ya Pili, Mwinyi mara baada ya sherehe za mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) cha jijini Dar es Salaam.kumalizika. |
Na Mwandishi Wetu
RAIS mstaafu wa
Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amewataka wahitimu wa vyuo
vikuu nchini kuacha tabia ya kuchagua kazi za kufanya mara baada ya
kuhitimu elimu yao. Mwinyi alisema tabia hiyo imepitwa cha wakati
hasa katika dunia ya sasa yenye changamoto kubwa ya ajira.
Rais Mwinyi alitoa
kauli hiyo juzi wakati akizungumza na wahitimu wa kozi mbalimbali
kwenye sherehe za mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU)
cha jijini Dar es Salaam.
Alisema kitendo
cha baadhi ya wahitimu hasa wa vyuo vikuu kupendelea kuchagua kazi za kufanya
kimekuwa kikiwapotezea muda na fursa anuai, hivyo kuwataka kuacha tabia hiyo
ambayo kwa kipindi hiki imepitwa na wakati.
Alisema wahitimu
hawana budi kuanza kufanya kazi zozote zinazojitokeza mbele yao na kutumia
fursa hiyo kuelekea kwenye mafanikio kadri walivyojipangia katika
maisha yao.
"...Nawapongeza
wahitimu kwa hatua hii, sasa mnaingia katika maisha mapya na ya vitendo msiende
kuchagua kazi za kufanya, anza na kazi yoyote inayojitokeza mbele
yako kisha uitumie
kutimiza ndoto zako," alisema katika hotuba yake kwa wahitimu hao.
Aidha Rais huyo
mstaafu aliwataka wahitimu hao kuwa wachapakazi, wabunifu na kutumia
ipasavyo ujuzi na elimu waliopewa katika ngazi mbalimbali ili
kuweza kuisaidia
jamii na taifa kwa ujumla.
Alisema kuwa
Serikali ya Tanzania imejipanga kuhakikisha wanafunzi wote wenye sifa na
vigezo vya kujiunga na chuo wanapata nafasi hiyo bila vikwazo
kupitia
Bodi ya Mikopo ya
Elimu ya Juu nchini (HESLB).
Akihimiza matumizi
ya lugha ya Kiswahili hasa kufundisha programu katika vyuo vikuu, Mwinyi
alivitaka vyuo vikuu kuanza kufundisha programu za lugha hiyo ili
kuchochea matumizi
yake kama yanavyofanya mataifa mengine kwenye vyuo vyao iwemo China,
Urusi, USA, Iran na mengineyo.
Alisema Afrika
lazima iwe na lugha moja ya kuwaunganisha watu wake na lugha pekee inayozungumzwa
na mataifa mengi ya Afrika ni Kiswahili hivyo kuna kila sababu ya
kujivunia lugha hiyo na kuitumia ipasavyo. "...Naahidi katika
mahafali yajayo nitatoa hotuba yangu kwa lugha ya Kiswahili na salamu
zangu zote nitazitoa kwa kiswahili," alisema Mwinyi.
Awali akizungumza
katika mahafali hayo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala (KIU),
Profesa Ndaula Muhammad alisema jumla ya wahitimu 1079 wamehitimu
masomo yao katika ngazi ya Shahada, Stashahada na Asatashahada katika
fani mbalimbali.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇