Afisa Habari wa Idara
ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Margareth
Chambiri (kulia) akiwakaribisha kwenye banda la Maonesho la NEC, Naibu Mawaziri
Mhe. Anthony Mavunde Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Vijana na
Mhe. Abdallah Possi (Mwenye Kofia) Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana
na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Wilayani
Bariadi mkoani Simiyu. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaendelea na program endelevu
za kutoa elimu ya mpiga kura kote nchini.
Naibu Mawaziri Mhe.
Anthony Mavunde Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Vijana na Mhe.
Abdallah Possi (Mwenye Kofia) Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu wakipata ufafanuzi kutoka kwa Maafisa wa NEC kuhusu
utendaji wa Mashine za BVR katika uchukuaji na uhifadhi wa taarifa za Wapiga
Kura leo kwenye maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Wilayani Bariadi –Simiyu.
Afisa TEHAMA wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Sanif Khalifan akitoa ufafanuzi kwa wanafunzi wa
Shule ya Sekondari Bariadi kuhusu taratibu za uchaguzi na hatua za uandikishaji
wa wapiga kura kupitia TEHAMA leo mjini Baridi wakati wa Tume hiyo ilipokuwa
ikitoa Elimu kwa Mpiga Kura kuhusu masuala mbalimbali.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇