MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO MUHESHIMIWA JOHN L. KAYOMBO |
Na Nassir Bakari
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Mh .John L.
Kayombo jana alitembelea na kukagua wodi mbalimbali za wagonjwa na kuzungumza na wafanyakazi wa hospitali ya Sinza
iliyopo Sinza Palestina.
Ziara hiyo imetokana na hatua ya Mkurugenzi kutaka kufahamu kero za wafanyakazi na miundo mbinu ya utoaji huduma ya hospitalini hapo.
“Nitaajiri watu wa Mifumo ya habari(IT), waje
watufunge mitambo ya kielektroniki itakayopunguza mianya ya wizi wa pesa,” alisema
Mkurugenzi Kayombo.
“Nimesikiliza kero zenu kwa umakini, naahidi kushughulikia moja baada ya nyingine na nawakaribisha ofisini kwangu muda wowote na kama kuna mfanyakazi ana tatizo lolote asisiste kuniambia," alisema Mkurugenzi Kayombo.
MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO MHESHIMIWA JOHN L. KAYOMBO AKIMSALIMIA MGONJWA ALIPOTEMBELEA WODI YA WAZAZI HOSPITALI YA SINZA. |
MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO MHESHIMIWA JOHN L. KAYOMBO KATIKATI AKIWA KWENYE KIKAO NA WAFANYAKAZI WA HOSPITALI YA SINZA. |
MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO MHESHIMIWA JOHN L. KAYOMBO AKITOKA NDANI YA CHUMBA CHA MKUTANO HOSPITALI YA SINZA. |
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇