Katibu
wa STDFAA, Jafari Makatu akizungumza
na waandishi wa habari leo
Jijini Dar es Salaam,
Kulia ni Mwenyekiti wa STFFAA, Ali Baucha na
kushoto ni Mdhamini
wa Chama hicho,
Ahmed Olotu.
|
Chama cha Waigizaji wa filam mkoa wa Kinondoni (STDFAA) wamemuomba Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuhimiza kukamilishwa Sera ya filamu ili ianze kutumika kuwasaidia wasanii katika mambo mbalimbali hususani ya kisheria.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu wa Chama hicho, Jafari Makatu alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na kuzungumzia changamoto zinazowakabili katika tasnia ya filamu nchini.
Makatu amesema kuwa Sheria ya Filamu ni muhimu katika tasnia hiyo hivyo ikiharakishwa itasaidia wadau wa tasnia hiyo kufanya kazi kwa uwazi na usalama wa hali ya juu kwa kuwa watakua wanalindwa na sheria.
“Tunamuomba Waziri wetu Mhe. Nape atuharakishie Sera ya Filamu kwa sababu sheria hiyo itatusaidia kuoanisha mambo mbalimbali ya kisheria kuanzia kwenye uandaaji wa kazi zetu hivyo, kupelekea kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa kazi bora zaidi”. Alisema Makatu../>>SOMA ZAIDI
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇