Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mrisho
Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ikulu jijini Dar es Salaam.
. Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika
picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja
na Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya tukio la Kiapo Ikulu
jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John
Kijazi wa kwanza (kulia) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jafo
wa kwanza (kushoto).
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara
baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
------------------
TAARIFA KAMILI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 19
Agosti, 2016 amemuapisha Bw. Mrisho Mashaka Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Kabla
ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Mashaka Gambo alikuwa Mkuu
wa Wilaya ya Arusha.
Bwana
Mrisho Mashaka Gambo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Daudi Felix
Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇