Mh.Mwigulu
Nchemba akizungumza na Makamu Mkuu wa chuo za SUA(Sokoine University of
Agriculture) alipofika kwaajili ya kukutana na wataalam,na uongozi wa
SUA kwaajili ya kupokea maoni yao kuelekea kilimo,ufugaji na uvuvi wa
kisasa. "Transformation of Agriculture".
Katika
kikao hicho,Wataalam kutoka SUA walisisitiza kuwa ili Tanzania iweze
kuondokana na kilimo holela,ni wakati muafaka sasa kama nchi kuamua
kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji na kuondoakana na kilimo cha
mvua,pia kuachana na jembe la mkono na wakati huo huo kuimarisha vituo
vya utafiti na kuzalisha mbegu kikanda.
Akiwa
njiani kuelekea Ifakara,Mwigulu Nchemba anaamua kufanya mkutao Jimbo la
Mikumi kijiji cha Tungu kwaajiliya kusikiliza kero za wananchi dhidi ya
uongozi wa miwa wilaya,Mkoa na Taifa,mahusiano mabaya ya kibiashara
kati ya wakulima wa miwana kiwanda cha ilovo,Lakini utitiri wa vyama vya
wakulima kwa eneo lakilombero.
Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mbunge wa Mikumi Mh.Joseph Haule(Prof.Jay) wakati wa mkutano huo
Baada
ya kusikiliza kero kutoka kwa wananchi na kusoma baadhi ya ripoti za
serikali ya wilaya na mkoa na zile za Tume mbalimbali zilizounda kujua
kiini cha matatizo ya wakulima wa miwa-Kilombero,Mwigulu Nchemba akiwa
ndiye waziri mwenye dhamana na kilimoa akaamua kufuta uongozi wote kwa
wakulima wa miwa kuanzia ngazi ya wilaya ya Mikumi hadi Taifa kwa kosa
la ubadhilifu na matumizi mabaya ya madaraka.
Mh.Mwigulu
Nchemba akiangalia mfereji ulioandaliwa kwaajili ya kusambaza maji
kwenye shamba la utafiti wa mbegu za Mpunga-Kilombero.Matumizi ya
mifereji kwenye kilimo yanaondoa mfumo wa kutegemea mvua ilimimea kupata
maji na kukua kwa wakati.
Mwigulu
Nchemba anatarajia kuendelea na ziara ya kukagua vituo vya Utafiti na
uzalishaji wa mbegu nchi nzima,lakini wakati huo huo atatembelea
mashamba ya mifugo na maeneo ya uvuvi wa samaki.
Picha/maelezo na festo Sanga Jr
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇