Mwenyekiti
mpya wa ccm mkoa wa Arusha Michael Lekule Laizer aliyepata kura 515akizungumza
mara baada ya kutangazwa mshindi wa kiti hicho hivi karibuni jijini
Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Katibu mwenezi wa chama hicho Mkoa wa Arusha Shabani Mdoe aliyeshinda
nafasi hiyo kwa kupata kura 36 ambaye kwa taaluma ni mwandishi wa
habari akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa mkutano huo mara baadaa
ya kutangazwa rasmi kushinda nafasi hiyo
Msimamizi
wa uchaguzi huo ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa Stephen
Wassiraakitangaza rasmi nafasi ya mwenyekiti wa mkoa ambapo pia
aliwataka wanaccm kuhakikisha wanashirikiana
Mjumbe
wa NEC Taifa toka wilaya ya Monduli Namelock Sokoine akizungumza katika
mkutano huo mara baada ya uchaguzi kuisha ambapo aliwataka wanaccm
kuchapa kazi na kuhakikisha wanawashuhulikia mamluki waliopo ndani ya
chama hicho
Mjumbe
wa NEC taifa toka wilaya ya Monduli Namelock Sokoine akiteta jambo na
Mbunge viti maalum Catherine Magige katika mkutano huo
Emanuel
Makongoro ambaye alikuwa akiwania nafasi wa uwenyekiti wa mkoa
akifurahia jambo na katibu wa wazazi mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau
Semi
Kiondo ambaye alikuwa akiwania nafasi ya ukatibu mwenezi akizungumza
mara baada ya uchaguzi kuisha ambapo alihaidi kutoa ushirikiano wake kwa
chama cha mapinduzi huku akishirikiana na viongozi waliochaguliwa
CHAMA cha Mapinduzi ( CCM)mkoa wa arusha kimefanya uchaguzi wa mwenyekiti wa mkoa na kufanikiwa kumchagua Maiko Lekule aliyepata kura 515 dhidi ya mgombea mwenza Emanuel Makongoro aliyepata kura 338,huku katibu mwenezi wa chama hicho akichaguliwa kuwa ni Shabani Mdoe aliyeshinda nafasi hiyo kwa kupata kura 36.
Aidha katika uchaguzi huo wa mwenyekiti wajumbe halisi waliopaswa kuhudhuria ni 960 ambapo waliohudhuria ni 903 huku wajumbe halisi waliopiga kura wakiwa ni 861.
Akitangaza matokeo hayo jana msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya ccm taifa Stephen Wassira alisema kuwa uchaguzi huo umefanyika kwa huru na amani na hivyo ana imani kuwa uongozi huo utakiletea mabadiliko makubwa chama cha mapindizi katika mkoa huo.
Alisema kuwa katika mkoa wa arusha matatizo ya umoja na tofauti yapo na kwamba atakayemaliza mzizi huo ni mwenyekiti aliyepatikana kwa kuhakikisha kuwa anawaunganisha wana ccm ili wawe kitu kimoja.
“hapa arusha yapo matatizo sana naomba tu nitumie fursa hii kumtaka mwenyekiti aliyeshinda kuhakikisha kuwa anakijenga chama na ndie atakayeifanya arusha iungwe mkono na watu wote hatutaki kusikia tena kuwepo kwa makundi ya kuvunja chama muda wa uongozi wa mwaka mmoja ni mkubwa sana katika kukirejesha chama sehemu yake”alisema Wassira.
Alileleza kuwa kwa arusha hawataki kusikia ccm inayoendeshwa kwa fedha ya mtu binafsi wala kampuni bali wanaitka ccm yao irudishe kwa wananchi na jamii iweze kunufaika na rasilimali zake sio kwa ajili ya watu binafs ambao ndio wamekuwa wakikisaliti chama.
Kwa upande wake mwenyekiti aliyechaguliwa Maiko Lekule akitoa neno la shukrani alisema kuwa anawashukuru wajumbe hao kwa kumchagua na kwamba nafasi aliyopewa hataweza mwenyewe kuimaraisha chama hicho ambacho kipo mahututi hivyo anaomba ushirikiano uwepo.
Lekule alisema kuwa chama hicho kinahitaji kufanyiwa ukarabati mkubwa sana hivo kamati za siasa ,wenyeviti na kamati inabidi waungane kwa pamoja kukijenga chama hicho kwa upya ili kirudi katia hali yake.
“mimi nahidi tu ntakiimarisha chama hiki kwa kushirikiana na wenzangu ila niwaombe tu mamluki wote walioko kwenye hiki chama ambao ndio wasaliti wakuu waondoke mapema wenyewe na kama hawataondoka tutawaondoa sisi”alisema Lekule.
Nae katibu
mwenezi Shabani mdoe ambaye ni mwandishi mwandamizi wa gazeti la Uhuru
aliwashukuru wajumbe hao kwa kumuamini kwa kumchagua na kuahidi kuwa
atatumia taaluma yake ya uhabari kuimarisha chama hicho kwani waandishi
wana nguvu kubwa ya kujenga palipobomoka.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇