Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni
Sefue akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam
wakati alipotangazia umma wa watanzania kuhusu hatua ambazo Rais Dk.
John Pombe Magufuli amechukua dhidi ya Dickson Mwaimu Mtendaji Mkuu wa
Mamlaka ya Taifa ya Vitambulisho vya taifa NIDA kutengua uteuzi wake na
kumsimamisha kazi mara moja pamoja na wasaidizi wake ambao ni Joseph
Makani Mkurugenzi wa TEHAM, Bi. Rahel Mapande Sfisa Ugavi Mkuu Bi.
Sabrina Nyoni Mkurugenzi wa Sheria na George Ntalima Afisa Usafirishaji
kwa kuwasimamisha kazi mara moja kupisha uchunguzi.
Taarifa zilizomfikia Rais
zinaonesha kuwa NIDA hadi sasa imetumia shilingi Bilioni 179.6 kiasi
hicho ni kikubwa na Rais angependa kufanyika uchunguzi na ukaguzi jinsi
fedha hizo zilivyotumika, maana Rais amekuwa akipokea malalamiko ya
wananchi kuhusiana na kazi ndogo ya utoaji wa vitambulisha vya taifa .
Hivyo Rais ameelekeza mamlaka ya
udhibiti wa manunuzi ya Umma PPRA wafanye ukaguzi wa manunuzi yote
yaliyofanywa na NIDA, TAKUKURU na CAG kufanya uchunguzi kwa pamoja ili
kubaini kama kulikuwa na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa taratibu au
la.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na
waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam , kulia ni Kaimu
mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano IKULU Bw. Gerson Msigwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇