- Kinana atembelea visiwa vya Iroba,Mazinga na Mulumo
- Aweka historia ya kuwa Katibu Mkuu wa kwanza kufika kwenye visiwa hivyo
- Asikitishwa na usumbufu unaofanywa na Sumatra kwa wavuvi
- Wananchi wamlalamikia kuhusu kujiandikisha kwa mbili,Mkuu wa Mkoa Kagera asema siku ni saba na ndio taarifa ya Serikali na sivinginevyo
- Wavuvi walalmikia suala la nyavu ,wasema kama ni haramu basi akamatwe anayeziingiza nchini.
- Kinana awataka viongozi wa CCM Muleba kushikamana na kuwa na umoja kati yao
Sehemu ya Kisiwa cha Bumbile pichani.
Bango la makaribisho ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwasili kwa boti kubwa ya Mv. Safari katika kisiwa cha Bumbile,wilaya ya Muleba mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakijaribu viatu vya mtumba kwenye soko la mtumba Iroba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kubeba matofali ya ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Iroba, iliyopo kisiwa cha Bumbile, Muleba mkoani Kagera.
Wakazi wa Kata ya Iroba wakiwa wamejikusanya kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mbunge wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka akizungumaz na wakazi wa kata ya Iroba kwenye uwanja wa michezo wa shule ya msingi Iroba.(Picha na Adam Mzee)
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Iroba kwenye viwanja vya shule ya msingi Iroba , Bumbile wilaya ya Muleba.(Picha na Adam Mzee)
Boti ndogo iliyombeba Katibu Mkuu wa CCM,Mbunge wa Jimbo la Muleba ya Kusini Profesa Anna Tibaijuka na Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella kutoka kisiwa cha Bumbile kuelekea Mazinga,wilayani Muleba.(Picha na Adam Mzee)
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiteremka kwa boti katika kisiwa cha Mulumo,wilayani Muleba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipunga mkono wakati akiwasili kwenye kisiwa cha Mulumo.(Picha na Adam Mzee)
Mbunge wa Muleba Kaskazini ambaye pia ni Naibu Waziri Nishati Charles Mwijageakicheza ngoma wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye kisiwa cha Mulumo, wilayani Muleba mkoani Kagera.(Picha na Adam Mzee)
Mbunge wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka akihutubia wakazi wa Muleba mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo Fatuma.(Picha na Adam Mzee)
Wananchi wa Muleba wakimsikiliza Mbunge wao Profesa Anna Tibaijuka wakati wa mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM ambaye yupo kwenye ziara ya kujenga na kuimarisha chama.(Picha na Adam Mzee)
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wakazi wa Muleba mjini waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya michezo Fatuma.(Picha na Adam Mzee)
Wananchi wa Muleba wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambapo aliwatahadhaisha vijana kuwa makini na makundi ya yanayoundwa na vyama vya upinzani kwani mengi yao yanaelekea kuwa na matendo ya kigaidi.(Picha na Adam Mzee)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Muleba mjini kwenye uwanja wa Fatuma ikiwa muendelezo wa ziara yake ya kujenga na kuimarisha chama,Kukagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi wa CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kijana Revocatus Mgunda cheti cha kuhitimu udereva wa bodaboda mabpo vijana zaidi ya 360 kutoka wilaya ya muleba wamefuzu mafunzo ya udereva wa boda boda ambayo yalidhaminiwa na mbunge wa jimbo hilo Profesa anna Tibaijuka .(Picha na Adam Mzee)
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwapungia mkono wananchi alipowasili kwa mtumbwi katika kijiji cha Katunguru, baada ya yeye na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kutembelea visiwa zaidi ya vinne, katika wilaya ya Muleba, leo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, na uhai wa Chama katika wilaya hiyo mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akimsikiliza kwa makini, Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofayika kijiji cha Katunguru, wilayani Muleba leo
Wananchi wa kijiji cha Katungulu wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowahutubia akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kukagua uhai wa CCM, mkoani Kagera.
Katibu wa NEC, Itkadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia wananchi katika Kijiji hicho cha Katunguru. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wananchi katika kijiji hicho cha Katunguru
Katibu Mkuu wa CCM, Abdlrahman Kinana akiwasili katika Uwanja wa Mpira wa Muleba Mjini, kuhutubia mkutano wa hadhara leo mchana
Katibu Mkuu wa CCM, Abdlrahman Kinana akiwasili katika Uwanja wa Mpira wa Muleba Mjini, kuhutubia mkutano wa hadhara leo mchana
Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage, akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera
Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera
KTIBU NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera
Uwanja wa mpira wa Muleba mjini, ukiwa umefurika wananchi wakati Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja huo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera
Katibu Mkuu wa CCM, akikabidhi cheti kwa mmoja wa maderefa wa bodaboda ambao wameshiriki mafunzo ya kuendesha bodaboda ambayo yaliratibiwa na Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka. Kinana alikabidhi vyeti hiyo katika mkutano huo wa hadhara
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimsikiliza kwa makini mkazi mmoja wa Muleba mjini, ambaye alikuwa na kero ambayo alitaka Chama Cha Mapinduzi kimsaidie kulitatua
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Profesa Anna Tibaijuka wakiwa na vijana wa bodaboda waliopewa vyeti baada ya kuhitimu mafunzo. (Picha zote na Bashir Nkoromo)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇