NA MATUKIODAIMABLOG
MKUU
wa mkoa wa Njombe Dr Rehema Nchimbi amempongeza mbunge Ludewa mkoani
Njombe Bw Deo Filikunjombe kwa kutumia sikukuu ya pasaka kuwaandalia
chakula watu wenye matatizo wakiwemo wafungwa wa gereza la Ludewa na
wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya wilaya ya Ludewa huku
akiagiza Halmashauri ya Ludewa kuanzisha huduma ya chakula kwa
wagonjwa .
Dr
Nchimbi alitoa pongezi hizo jana wakati alipoungana na mbunge huyo
na viongozi mbali mbali wa mkoa na wilaya ya Ludewa kushiriki
hadla hiyo ya mbunge kula chakula pamoja na wagonjwa na kuwapa
misaada mbali mbali kama ulivyoutaratibu wake kwa kila sikukuu kula
na wagonjwa na wafungwa .
Alisema
utaratibu unaotumiwa na mbunge huyo ni utaratibu mzuri ambao
unapaswa kuigwa na wabunge wengine nchini kwa kuyatembelea makundi
mbali mbali ya kijamii wakati wa sikukuu ama siku nyingine badala ya
kusherekea sikukuu kwa kufanya anasa.
'kweli
ni jambo la kumpongeza sana mbunge Filikunjombe kwa huu utaratibu
ambao amekuwa akiufanya binafasi niliposikia mbunge anakuja kufanya
jambo hili kubwa la kula na wagonjwa pasaka niliamua kufunga
safari na mimi kuja kushiriki zoezi hili na kumtia moyo zaidi
mbunge kwa hili si wabunge wote ambao wanakawaida ya kutembelea
na kuwafariji wagonjwa na wafungwa kama hivi 'alisema mkuu huyo
Hata
hivyo mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa katika kumuunga mkono
mbunge Filikunjombe kwa wazo hilo zuri kwa upande wake
anachangia ngunia 5 za mahindi ili kuwaanzishia wagonjwa wanaofika
kujifungua huduma ya chakula kwa kipindi chote wawapo hospitalini
hapo kama njia ya kuepusha wagonjwa kuwa na mawazo ya wapi
watapata chakula
kwani
alisema si wagonjwa wote wanaofika kusubiri muda wa
kujifungua hospitalini hapo wanauwezo wa kiuchumi hivyo kuiagiza
halmashauri ya wilaya ya Ludewa kuangalia uwezekano wa
kuchangisha chakula kwa wananchi ili kusaidia huduma ya chakula kwa
wagonjwa .
Alisema
wilaya ya Ludewa na mkoa wa Njombe kwa ujumla hauna shida ya chakula
kama ilivyomikoa mingine hivyo uwezekano wa kuanzisha utaratibu
wa kutoa chakula kwa wagonjwa unawezekana .
Akishukuru
kwa msaada huo wa chakula kwa niaba ya wagonjwa wengne waliolazwa
hospitalini hapo paroko wa kanisa la anglikana ludewa Andrew
Hiluka alisema kuwa alichokifanya mbunge huyo ni moja kati ya
baraka kubwa kwake na kuwa baadhi ya wanasiasa wanapoteza nafasi
zao kutokana na kuwa na roho mbaya na uchoyo kwa wale
waliowachagua.
Kwani
alisema Ludewa imepata kuwa na wabunge zaidi ya watano ila
wakati wa sikukuu kama hizo wabunge hao walikuwa wakitoka nje ya
Ludewa ama kujifungia na familia zao kula sikukuu tofauti na
Filikunjombe ambae amekuwa ni mbunge wa aina yake kwa siku ya
sikukuu kuandaa chakula cha pamoja na wagonjwa kwa kula nao chakula
wodini .
Paroko
Hiluka alitoa wito kwa wananchi wa jimbo la Ludewa kuendelea
kumchangua kwa miaka mingine zaidi mbunge Filikunjombe kwani
ametambua mahitaji sahihi ya wana Ludewa kwa kusaidia maendeleo
ya jimbo hilo pia kuwagusa wote wenye matatizo mbali mbali ambao
ni nje ya ahadi zake za ubunge .
Alisema
ni kipindi cha Filikunjombe kasi kubwa ya maendeleo imeonekana
kwa kila mwananchi wa wilaya hiyo na nje ya wilaya lakini pia ni
mbunge pekee kusomesha sekondari watoto yatima zaidi ya 700
katika wilaya hiyo kwa kila mwaka huku wabunge waliopita labda
aliyejitiahidi kusomesha basi haikuzidi watoto 2 kwa miaka yote mitano
.
Nae
mbunge Filikunjombe alisema kuwa utaratibu huo wa kula chakula
na wagonjwa amekuwa akiufanya kila mwaka toka alipoingia madarakani
mwaka 2010 na kuwa iwapo wananchi wa jimbo hili watamchagua
ataendelea kuwaletea maendeleo lakini pia kuwasaidia watu wenye
matatizo kwani anachoamini na kuendelea kuamini kuwa wazima na
wagonjwa wote ni wapiga kura wake na kuwa furaha yake ni kuona
wagonjwa wanapona ili waweze kumchagua tena.
|
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇