Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kulia akikabidhi msaada wa mataulo na mito kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Wiliam Waziri kwa ajili ya Hospitali ya wilaya ya Ludewa
Mbunge wa Ludewa akizungumza na watumishi wa Hospitali ya wilaya ya Ludewa |
Watumishi wa Hospitali ya wilaya ya Ludewa wakimshangilia mbunge wao Deo Filikunjombe kwa msaada Hospitalini hapo |
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akionyesha mataulo ya kisasa |
Watumishi wa Ludewa Hospitali wakimsikiliza mbunge wao |
mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe kushoto akishiriki kushusha shehena na vifaa mbali mbali alivyovitoa katika Hospitali ya wilaya ya Ludewa |
Filikunjombe mwenye T-Shet ya CCM akisaidiana na watumishi wa Hospitali ya wilaya ya Ludewa kushusha vifaa mbali mbali |
Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe mwenye T-Shet ya CCM kulia akisaidiana na watumishi wa Hospitali ya wilaya ya Ludewa kushusha vifaa mbali mbali |
Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya wa tatu kushoto akisaidia kushusha mizigo |
Vitu vilivyotolewa na Filikunjombe |
Mbunge Filikunjombe akifurahi jambo wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Ludewa mara baada ya kukabidhi misaada mbali mbali |
Na FG Blog, Ludewa
KATIKA kukabiliana na tatizo la uhaba wa vifaa mbali mbali katika Hospitali ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe mbunge wa Jimbo la Ludewa (CCM) Deo Filikunjombeamekabidhi msaada wa Mashuka ya wagonjwa 200, Blanketi ya kisasa 100,taulo za kuogea wagonjwa 200 pamoja na mito 100 ya kulalia wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya milioni 32 .
Mbunge huyo amefikia hatua hiyo kutokana na tatizo kubwa la Hospitali hiyo kukabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo na vifaa hivyo kwa wagonjwa .
Akikabidhi msaada huo hospitalini hapo jana mara baada ya kuzungumza na watumishi wa sekta ya afya Mbunge huyo ,aliwataka watumishi hao kuwa waaminifu kwa kuviangalia vifaa hivyo visipotee na badala yake wavitunze na vitumike kwa ajili ya wagonjwa na si vinginevyo .
Alisema,anathamini na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na watumishi hao katika kuwahudumia wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo lakini amewataka kuthamini wapiga kura wake hao kwa kuwapatia huduma inayostahiri na kuokoa maisha yao.
“Nawaomba sana ndugu zangu watumishi mjitahidi kutunza hivi vifaa nilivyoleta ilimnitie moyo niendelee kusaidia zaidi ,kwani hii ni fedha yangu binafsi niliyokaata kwenye posho yangu ya vikao vya bunge pia naomba muithamini sana kazi yenu ,kwani ajira ni ngumu na kuna watu wanahangaika huko mitaani kutafuta ajira pamoja na usomi wao hakuna ajira, tuwatumikie wagonjwa kwa upendo na furaha ikiwa ni pamoja na kuhokoa maisha yao kwani wanachohitaji toka kwenu ni upendo na huduma nzuri tu,alisema Filikunjombe.
Awali akisoma Risala fupi ya hospitali hiyo kwa Mbunge huyo Kaimu Mganga mkuu Hospitali ya Wilaya ya Ludewa Apolnary Nombo alisema,
Watumishi hao wanaheshimu jitihada kubwa ambazo amezifanyahususani kwenye sekta hiyo katika kipindi cha miaka mitano ainaonekana na zinapimika ndani na nje ya Bunge ikiwa ni pamoja na kuwatembelea mara kwa mara na kutoa misaada hospitalini hapo.
Hata hivyo alisema bado hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali ambazo zinakwamisha maelengo yao ikiwemo ya kukosekana vifaa muhimu katika jengo la upasuaji ikiwemo mashine ya kuchemshia vifaa vya upasuaji na mashine za kutolea dawa za usingizi .
Pia changamoto nyingine ni uchakavu wa jengo la wazazi ambao unapingana na MDG 4 na 6 upunguzaji wa vifo vya wazazi pamoja na ukosefu wa chumba cha watoto wachanga ambao wakizaliwa njiti wanahitaji huduma hiyo pamoja na changamoto nyingine ambazo waliomba msaada wa mbunge huyo .
Mganga huyo alipongeza jitihahada mbali mbali ambazo zimekuwa wakifanywa na mbunge Filikunjombe katika Hospitali hiyo na Zahanati za vijiji mbali mbali katika wilaya ya Ludewa na kuwa pasipo kuboresha huduma za afya kwenye zahanati hizo yawezekana idadi ya wagonjwa kukimbilia katika Hospitali hiyo ya wilaya ingekuwa kubwa zaidi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇