TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu
Mkuu wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Ndugu Sixtus Mapunda
anategemea kufanya ziara ya siku na nne (14) katika mikoa minne ya
Kanda ya Ziwa, ambayo ni Tabora, Shinyanga, Geita na Kagera kuanzia
kesho tarehe 12st Dec 2014.
Ziara
hii ya kikazi ya Katibu Mkuu inalenga kukagua na kuhimiza ujenzi na
uimara wa jumuia ya Vijana katika maeneo husika lakini pia kushiriki
kampeni zinazoendelea za uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa
kufanyika mnamo tarehe 14th Dec 2014.
Pia,
Katibu Mkuu anatarajia kufanya mikutano ya ndani na viongozi wa
Jumuiya na Chama, pia kufanya mikutano ya hadhara inayolenga
kuingiza wanachama wapya ndani ya jumuiya na chama kwa ujumla.
Kuhimiza
wanachama wa chama cha mapinduzi na viongozi kuwaandaa wananchi
katika kuipigia kura katiba mpya iliyopendekezwa wakati ukifika.
Ziara
hiyo ya Katibu Mkuu inategemea kumalizika tarehe 25th Dec
2014.
Kidumu
Chama Cha Mapinduzi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇