LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 11, 2014

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AFUNGUA KONGAMANO LA UFUGAJI NYUKI AFRIKA LEO JIJINI ARUSHA

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama ngoma alipowasili kufungua kongamno la ufugaji nyuki Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) leo Novemba 11, 2014. Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wapili kushoto) na Wahadzabe kutoka wilaya ya Mkarama Singida, Waidona Wazael (kulia) na mwanae Jacob Edward  katika kongamano la Ufugaji Nyuki Afrika lililofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) Novemba 11, 2014.
  Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akitazama mazao mbalimbali yanayotokana na nyuki katika maonyesho yaliyokwenda sambambamba na Kongamano la  Ufugaji Nyuki Afrika  kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Novemba 11, 2014. Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na kushoto kwake ni Mhamasishaji wa ufugaji nyuki na usindikaji asali  wilayani Loliondo, Krystern Erickson.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaonyesha wazee wa kabila la Wahadzabe asali iliyofungashwa tayari kwa kuuzwa katika Kongamano la Ufugaji nyuki barani Afrika lililofanyika kwenye  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa chaArusha ( AICC)  Novemba 11, 2014. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Vincent Ole Kone, wapili kulia ni Maidona Wazael  na watatu kulia ni Jacob Edward.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea tuzo ya Uhamasishaji na Ufugaji bora wa nyuki  kutoka kwa Rais wa Chama cha Wafugaji Nyuki Duniani, Gilles  Ratia  katika kongamani la ufugaji nyuki barani Afrika lililofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Novemba 11, 2014. Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akionyesha  tuzo ya Uhamasishaji na Ufugaji bora wa nyuki  aliyokabidhiwa na  Rais wa Chama cha Wafugaji Nyuki Duniani, Gilles  Ratia  (kushoto)  katika kongamano la ufugaji nyuki barani Afrika lililofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha  Kimataifa cha   Arusha (AICC) Novemba 11, 2014. Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia  wakati alipofungua Kongamano la Ufugaji Nyuki Barani Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Novemba 11, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusu vifaa vya kukamulia asali kutoka kwa watalaam wa Kichina, Huang Hejie (kushoto) na  Zhinyong Wang (watatu kushoto) katika kongamano la Ufugaji Nyuki Afrika  lililofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha  (AICC) Novemba 11, 2014.(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages