Katibu Mkuu wa CCM atakuwa kwenye ziara ya siku mbili ndani ya wilaya ya Simanjiro kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi wa CCM mwaka 2010 na kukagua uhai wa Chama.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kitwai A ambapo aliwashukuru wananchi kwa kushirikiana na CCM.Kinana amekuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa CCM kufika kijijini hapo.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Ndugu Christopher Ole Sendeka akihutubia wananchi wa kijiji cha Kitwai A ambapo aliwahakikishia wananchi hao kuwajengea shule ya sekondari na kujengewa mnara wa simu kwa ajili ya mawasiliano pamoja na umeme.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mbunge wa Jimbo la Simanjiro CCM Ndugu Christopher Ole Sendeka kwa pamoja wamepewa heshima na Wazee (Ole Guanan) wa kijiji cha Kitwai na kutambulika kama Ole Kinana, Ole Nape na Ole Sendeka.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇