Gari aina ya RAV4 ikiwa chali baada ya Kupata ajali mbaya Maeneo ya Kibaigwa ukiwa uanelekea Mkoani Dodoma.Mh:Mwigulu Nchemba akisaidia kuoka Majeruhi kwa Kuinua gari.Gari aina ya RAV4 ikiwa imeshainuliwa tayari na Majeruhi wametoka walikuwa wawili.Kazi ya Kuondoa Betri ya Gari ndio inafanyika ilikuepusha Moto.Huyu ndiye alikuwa Dreva wa gari hii iliyopata ajali,amepata Michubuko kidogo.Ajali
ndogo Imetokea maeneo ya Kibaigwa ikihusisha gari aina ya RAV4
iliyokuwa ikitokea Mkoani Morogoro kwenda Dodoma,Ajali hiyo mbayo
haijasababisha Kifo chochote imetokea majira ya Mchana wa Tar.08/06/2014
na Sababu ya ajali inatajwa kuwa ni Mwendo kasi wa Dreva na hatimaye
Gari Kumshinda na kupinduka.
Katika
hali ya Kuonesha Ubinadamu na Utu kwa Watu Wengine,Mh:Mwigulu Nchemba
aliyekuwa akitoka Dodoma kuelekea Morogoro kwenye Mkutano alilazimika
Kusimama kwa Muda kwenye ajali hiyo kwaajili ya Kutoka Huduma ya Kwanza
kwa Majeruhi kama anavyoonekana Pichani hapo Juu.Jambo hilo
liliwafurahisha sana Wananchi waliokuwa eneo la ajali na waliomba
Viongozi wengine waige tabia hii ya Mwigulu Nchemba ya Kushirikiana na
Wananchi wakati wa Shida husuasani wanapoona ajali
barabarani,Ugonjwa,Misiba n.k wajitahidi kutoa Ushirikiano.
Picha/Maelezo na Sanga Jr
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇