NA MWANDISHI MAALUM, USA
Msanii mkongwe wa kuchezea nyoka, Salima Moshi, amesema Balozi zina nafasi nzuri za kuutangaza utamaduni wa Tanzania nje ya nchi kwa kuwa wapo karibu na nchi husika.
Amesema kutokana na ukaribu huo mabalozi wanaweza kujenga mazingira ya kuviwezesha vikundi kwenda kufanya maonyesho katika nchi hizo za nje.
Salma amesema hayo alipokwenda kumuona Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Liberata Mulamula, kwa ajili ya kumsalimia na kuwa na mazungumzo.
Msanii huyo ambaye kwa sasa anaishi Marekani, pia aliomba BARAZA LA SANAA LA TAIFA kuandaa kitabu kitakachojumuisha wasanii mbalimbali na anwani zao vitabu hivyo vipelekwe kwenye balozi zetu ili watu mbalimbali wanaokuja waweze kuvisoma na hatimaye kuwaalika wasanii wataweza kuutangaza utamaduni wetu na wasanii kujipatia kipato na pia kujifunza.
Alisema mapromota wengi baada ya kupata wamekuwa wanawatelekeza wasanii na pato kubwa linaenda kwao bila kunufaisha msanii na hata wale wanaobahatika kupiga sanaa zao nje ya Tanzania wamekuwa wanaishia kuwapigia Watanzania ifike wakati wakiwa nchi za nje waweze kutumbuiza na wenyeji huku akitoa mfano kama JZ aende Tanzania halafu awapigie Wamarekani.
Salima alikemea vikali swala la kukopi kazi za sanaa linarudusha nyuma maendeleo ya wasanii na aliomba Serikali kutoa adhabu kali kwa watakao bainika na kusimamia swala la hakimiliki.
Msanii huyo mkongwe alisema imefika wakati sasa wasanii kuwa na wanasheria hali ambayo itasaidia kulinda haki zao.
Salima alimshuru sana Rais Jakaya Kikwete akisema amekuwa wakati wote karibu na wasanii na hata hivi karibuni aliwaalika kwenye chakula cha jioni na kuomba nafasi hiyo wasanii waitumie vizuri.
Alisema kuhusu tunzo ziwe zinatoa kwa wasanii wa sanaa za maonyesho na wakati umefika kutoa kibali kwa waandaaji wengine si vibaya zikawa zaidi ya moja pia aliombakusaidia kujenga maktaba kwenye eneo la viwanja vya wasanii Mkuranga na kumpongeza Mwenyekiti wa wasanii bw Twalibu.
Balozi Mulamula alimshukuru sana msanii huyo na kumpongeza kwa kazi nzuri ya kuwakilisha nchi na kuwa msanii atakayekuwa mfano kwa wengine.
Alisema kuhusu Hakimiliki Serikali imejizatiti kikamilifu kuhakikisha haki za msanii zinalindwa alisema ni vyema wasanii wakajua haki zao hii itawasaidia sana aliongolea mapromota ni vyema kuangalia maslahi ya wasaniikwanza MH Balozi alisifu sana kazi zinazofanywa na wasanii mbalimbali nchinina kuitangaza nchi
Msanii wa siku nyingi wa kuchezea nyoka, Salma Mosha (kushoto) akizungumza na
Balozi wa Tanzania nchini Mrekani, Balozi Liberatha Mulamula, alipoenda
kuzungumza na balozi hiyo ofisini kwake nchini Marekani.
Your Ad Spot
Feb 21, 2014
Home
Unlabelled
SALMA MOSHA: BALOZI ZINA NAFASI KUBWA YA KUTANGAZA UTAMADUNI WA TANZANIA KIMATAIFA
SALMA MOSHA: BALOZI ZINA NAFASI KUBWA YA KUTANGAZA UTAMADUNI WA TANZANIA KIMATAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇