Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimsalimia Katibu Mkuu wa Chama cha ANC cha Afrika Kusini, Gwede Mantash, kabla ya chakula cha jioni alichowaandalia Makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika, jana, Oktoba 9, 2013, Ikulu jijini Dar es Salaam, Makatibu wakuu hao walikwenda Ikulu baada ya mkutano wao wa sita, uliofanyika hapa nchini. Wapili kushoto ni Julio Paulo, Katibu Mkuu wa Chama cha MPLA cha Angola na kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China, Ai Ping na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika, kabla ya kula nao chakula cha jioni, Ikulu jijini Dar es Salaam, Oktoba 9, 2013. Kutoka kushoto na vyama vyao vikiwa kwenye mabano makatibu wakuu hao ni, Nangolo Mbumba (SWAPO) cha Namibia, Gwede Mantash (ANC) cha Afrika Kusini, Didy Mutasa (ZANU-PF) Zimbabwe, na kutoka kulia ni Abdulrahman Kinana (CCM) Tanzania, Philipe Paunde (FRELIMO) Msumbiji na Julio Paulo (MPLA) Angola.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisisitizia jambo, Makatibu Wakuu wa vyama vilivyokuwa vya Ukombozi Kusini Mwa Afrika, alipokutaja nao kwa ajili ya chakula cha jioni, alichowaandalia, jana, Oktoba 9, 2013, Ikulu jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto na vyama vyao vikiwa kwenye mabano makatibu wakuu hao ni Gwede Mantash (ANC) cha Afrika Kusini, Didy Mutasa (ZANU-PF) Zimbabwe, na kutoka kulia ni Abdulrahman Kinana (CCM) Tanzania, Philipe Paunde (FRELIMO) Msumbiji na Julio Paulo (MPLA) Angola.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza na ujumbe wa Makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika, wakati wa chakula cha jioni alichowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam, jana, Oktoba 9, 2013.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza na ujumbe wa Makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika, wakati wa chakula cha jioni alichowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam, jana, Oktoba 9, 2013.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, CCM, Zakiah Meghji, wakati wa chakula cha jioni alichowaandalia makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika, jana, Oktoba 9, 2013, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akimtambulisha Katibu Mkuu wa Chama Cha MPLA cha Angola, Julio Paulo, kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam, jana, Oktoba 9, 2013.
Katibu Mkuu wa chama tawala cha Afrika Kusini ANC, Gwede Mantash (kushoto) akimpa zawadi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, mwishoni mwa mkutano wa sita wa Makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika, jana, Oktoba 9, 2013, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipewa zawadi Katibu Mkuu wa chama cha SWAPO cha Naimibia Nangolo Mbumba, mwishoni mwa mkutano wa sita wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika, jana, Oktoba 9, 2013, jijini Dar es Salaam.
Your Ad Spot
Oct 10, 2013
Home
Unlabelled
MWENYEKITI WA CCM, RAIS JAKAYA KIKWETE ALA CHAKULA CHA JIONI NA MAKATIBU WAKUU WA VYAMA VILIVYOKUWA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
MWENYEKITI WA CCM, RAIS JAKAYA KIKWETE ALA CHAKULA CHA JIONI NA MAKATIBU WAKUU WA VYAMA VILIVYOKUWA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇