LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 12, 2013

KISHAPU WASEMA WAO NI CCM TU INATOSHA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi waliofika kumpokea kwenye wilaya ya Kishapu katika eneo la Maganzo ambapo Katibu Mkuu alikuwa na ziara katika wilaya ya Kishapu.

 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahma Kinana akichekecha mchanga wa kujengea darasa katika shule ya sekondari ya Mwigumbi,Katibu Mkuu amekuwa akishiriki katika shughuli za kijamii hasa zinazohusu utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa CCM.

Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi moja ya madarasa katika shule ya Sekondari Mwigumbi.

Moja ya Nyumba mpya iliyojengwa kwa ajili ya makazi ya Walimu wa Shule ya Sekondari Mwigumbi, wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga ambayo ilizinduliwa leo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitumia usafiri wa baiskeli kufika kijiji cha  Mwigumbi ambapo kulikuwa na shughuli za kuzindua mradi wa maji.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kuzindua mradi wa maji wa kata ya Mondo,kijiji cha Mwigumbi wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha maji mkazi wa kata ya Mondo,kijiji cha Mwigumbi kama ishara ya kuzindua mradi wa maji ,Huu ndio utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ambao wilaya ya Kishapu inafanya vizuri.
 Mbunge wa Kishapu Suleiman Masoud Mchambi akishiriki kucheza ngoma ya kiasili wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji uliofanyiaka kata ya Mondo kijiji cha Mwigumbi.
 Tanki la maji litakalowasaidia wakazi zaidi ya 4000 katika kijiji cha Mwigumbi ,pichani wakazi wa kijiji hicho wakiwa wamekusanyika kushuhudia uzinduzi rasmi wa tanki hilo.

 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mwigumbi mara tu baada ya kuzindua mradi wa maji utakaosaidia zaidi ya watu 4000.
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Ndugu Azah Hilal Hamad akiwahutubia wakazi wa kata ya Mondo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Mwigumbi.
 Mbunge wa Kishapu Ndugu Suleiman Masoud Mchambiakihutubia wakazi wa kata ya Mondo na kuelezea namna gani jimbo lake limekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiingia kwenye viwanja vya Mabela kwa staili ya aina yake tayari kuhutubia wakazi wa Wilaya ya Kishapu.

 Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akimtambulisha Balozi wa China Lu Youqinq kwa wakazi wa wilaya ya Kishapu na kuwaambia neema inakuja kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga kwani China itawekeza kwenye viwanda vya Pamba .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza  Balozi wa China hapa nchini ndugu Lu Youqinq wakati wa mkutano wahadhara uliofanyika katika viwanja vya Mabela, kushoto kwake ni Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akicheza ngoma pamoja na Balozi wa China LU Youqinq leo kwenye viwanja vya Mabale,Wilaya ya Kishapu.

  Balozi wa China nchini Lu Youqinq akionyesha ujuzi wa kucheza ngoma za asili za Kitanzania  mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.
 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea taarifa za maendeleo ya ujenzi wa hospital ya wilaya ya Kishapu,Katibu Mkuu ameongozana na Balozi wa China Lu Yuoqinq katika hospitali hiyo ambapo Balozi nae ameahidi kusaidia kwenye sekta hiyo muhimu ya afya.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages