serikali ya wilaya ya kilwa imewataka wazazi na walezi wanaotakaza
watoto wao kwenda shule wachukuliwe hatua za sheria ili kukomesha
vitendo hivyo.
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya Kilwa Abdala Ulega wakati
alipokuwa anazungumza na wazazi walezi na wadau wa elimu wa shule ya
sekondari mibuyuni wilayani humo jana.
Ulega alisema kufanya hivyo sio tu kwamba ni kuwa nyanyasa bali pia
ni kuwanyima hakiyao ya msingi na urithi wa maisha yao ya baadaye
watoto ambao ndiyo tegemeo la taifa.
Watendaji wa tarafa, kata, kijiji wametakiwa kutekeleza agizo hilo
kwa kuwachukulia hatua wazazi na walezi aina hiyo.
Alisema kuwa kuwakataza watoto kwenda shule mbali na kuwanyima haki
zao vilivile kunakwamisha juhudi za serikali za kukuza elimu.
Ulega alitoa agizo hilo baada ya kupata taarifa kuwa zaidi ya watoto
200 wa shule ya sekondari Mibuyuni hawafiki shuleni kutokana na utoro
wa rejareja na kusababisha shule hiyo kuwa na mahudhurio madogo kila
siku.
Aidha shule ya sekondari mibuyuni ambayo iko katika wilaya Kilwa
Mkoani Lindi ni kati ya shule 10 zilizofanya vibaya katika matokeo ya
kitado cha nne mwaka huu.
HONGERA SANA DC ULEGA Ila jukumu kubwa ni kuhakikisha Bwege anarudisha Ubunge kwa CCM na Idadi ya madiwani,Mitaa,Vijiji vingi virudi..SAWAAA!!!! KAIDI UONE
ReplyDeleteHONGERA SANA DC ULEGA Ila jukumu kubwa ni kuhakikisha Bwege anarudisha Ubunge kwa CCM na Idadi ya madiwani,Mitaa,Vijiji vingi virudi..SAWAAA!!!! KAIDI UONE
ReplyDelete