Mawaziri
wa Fedha, Kilimo, Uchukuzi, Maji, Nidhati na Madini na Elimu wakiweka
saini waraka wa kujifunga katika utekelezaji wa mfumo mpya wa
kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo
uliokabidhiwa kwa wizara sita hizo sita baada ya semina elekezi kwa
mawaziri na makatibu wakuu iliyofanyika ukumbi wa St Gaspar mjini
Dodoma. Mfumo huo unaanza kutekelezwa kwa kutumia uzoefu wa Performance
Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia. Mfumo huu
utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President’s Delivery Bureau (PDB)
ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili
kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Awamu ya kwanza
ya labs ilizinduliwa rasmi na Rais Kikwete tarehe 22 Februari, 2013 na
kumalizika mwezi huu wa Aprili, 2013. Maeneo ya awamu ya kwanza ya labs
yanahusisha elimu, kilimo, nishati, mapato, maji na miundombinu ya
uchukuzi.
|
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇