Kutoka LINDI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi Taifa Ndugu Jakaya M. Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoani
Lindi ambapo amehudhuria Maazimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, ambapo kitaifa
yamefanyika Mkoani hapa na pia anakagua na kufuatilia mipango na miradi
mbalimbali ya Maendeleo.
Miongoni mwa Miradi aliyozindua ni pamoja na Daharia ya Shule ya
Wanawake Nachingwea iliyopo eneo la Bomani wilayani Nachingwea. Shule hiyo
maaalum ya Wanawake imejengwa kwa nguvu za Wananchi wa Nachingwea wenyewe kwa
kuchangishana kwa kushirikiana na Serikali.
Ujenzi wa Shule hiyo ulianza 2010 kutoka katika ruzuku ya Serikali
katika mpango wa Serikali kuwainua na kuwawezesha wanawake kwa kuwapa fursa za
Elimu kwa kuangalia namna ya kukabiliana na Changamoto zinazowakabili watoto wa
kike, kama mimba za utotoni,umbali na mkakati wa kuongeza idadi ya watoto wa
kike mashuleni.
Mheshimiwa Rais alitoa msaada wa pesa taslimu na ahadi ya kujenga
Maabara, Viwanja vya michezo, Uzio, Jengo la Utawala, Bweni na Kuongeza Idadi
ya Walimu. Pia aliipongeza Halmashauri ya wilaya hiyo kwa kupata wazo la
kuendeleza majengo yaliyoachwa magofu kwa kutengeneza Shule hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇